*********************************
Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma ameutaka uongozi wa chuo cha uongozi wa mahakama lushoto[ IJA ] kuhakikisha wahitimu wanaomaliza chuoni hapo kumudu matumizi ya
tehama pamoja na kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao ili kuingia katika kazi ya ushindani.Ameyasema hayo katika mahafali
ya ishirini chuoni hapo yakiwa yameambatana na maadhimisho ya kilele
cha miaka 20 toka kuanzishwa kwa chuo hicho.
Profesa Ibrahimu amesema
wanafunzi wanaotokana na chuo hicho lazima wawe wanafunzi wa karne ya 21
na karne ya 21 inaongozwa na wanawake tofauti na karne zilizopita
ilikuwa zikiongozwa na wanaume.
Hivyo amewataka wajaribu
kuwapandisha wanafunzi wa astashahada na stashahada ili wawe sambamba na
mapinduzi makubwa yanayoendelea katika matumizi ya tehama katika huduma
mbalimbali.
;wahitimu wenu lazima wafahamu
namna kanuni za ufunguaji wa mashauri kwa njia ya elecronic zinazotumika
kila siku mahakamani ili wawe wanafahamu namna gani tehama inatumika
mahakamani; Alisema Profesa Ibrahimu.
Nae Mwenyekiti wa baraza la
uongozi wa wa chuo Dkt Gerald Ndika amesema tafiti mbalimbali za
wataalamu wa uchumi duniani zinaonyesha kuwa nchi ambazo uchumi wake
umekuwa kwa kiasi ni nchi ambazo zimewekeza zaiodi kwenye maarifa na
ujuzi.
Amesema chuo kimeendea kufanya
vizuri katika technologia ya habari ya mawasiliano tehama kwa kuakisi
hilo chuo kimeendelea kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana
na taasisi nyingine za kimataifa ikiwemo taasisi ya mafunzo na utafiti
ya umoja wa mataifa [united nations institute for trainning and research
-unitar] iliyopo uswisi.
Pia Dkt Ndika ameeleza kuwa
zimekuwepo juhudu zinazofanywa na uongozi wa chuo katika kukarabati
majengo yaliyopo ili kukidhi mahitaji na nyezo za ufundishaji na huduma
bora kwa wanachuo na wafanyakazi.
;Pamoja na hatua iliyofikiwa na
uongozi wa chuo katika ukarabati wa majengo yapo maombi ya kuendeleza
kazi hiyo pamoja na kutafuta ufadhili ya kufanikisha malengo mengine ya
chuo; Alisema mwenyekiti huyo.
Mkuu wa hicho Dkt, Paul Kihwelo
alisema licha ya mafanikio yaliyopo chuoni hapo katika ngazi ya
stashahada na astashahada chuo kimeendelea kutekeleza kwa vitendo
malengo ya kuanzishwa kwake kwa kutoa mafunzo elekezi kwa watumishi wa
mahakama ngazi mbal;imbali ikiwemo majaji wa mahakama kuu na mahakama ya
rufani lakini pia mahakimu wapya.
Dkt Kihwelo amebainisha kwamba
katika miaka ya hivi karibuni chuo kimejihimalisha katika kutoa ushauri
[consultancy]pamoja na uitafiti sasa chuo kinamiradi kadhaa.
No comments :
Post a Comment