Wednesday, December 30, 2020

Ruzuku ya Milioni 398.8 kutoka COSTECH yatumika kujenga maabara ya kudhibiti ubora wa achanjo za mifugo- TVLI-Kibaha


Mkurugenzi wakituo cha TVLI_Kibabha akizungumza kuhusu kituo hicho kinavyofanya kazi.
Mkuu wa Kituo cha TVLI_Kibaha Dr Stela Bitanyi akionyesha nanna bora ya kuhifadhi sampuli za chanjo za mifugo.

TAASISI ya Utafiti wa Chanjo za Mifugo Tanzania (TVLI) Kibaha iliyopo chini ya Wakala wa Maabara ya Utafiti wa Mifugo (TVLA) ilianzishwa mwaka 2012 ikiwa na jukumu la kuhakikisha inadhibiti magonjwa ya mifugo yaliyopewa kipaumbele nchini.

Katika utekelezaji wa majukumu yake imekuwa ikikumbana na changamoto ya upungufu wa vifaa kwa maabara yenye ubora wa kusaidia udhibiti wa chanjo za magonjwa ya kimkakati, kwa miaka ya hivi karibuni Taasisi ilikuwa inazalisha chanjo mbili (2), na kwa sasa imefikisha chanjo sita (6) huku kukiwa na mkakati wa kufikisha chanjo nane (8) mpaka kumi na tatu (13) kwa mwaka 2022.
Mwaka 2018, Taasisi ya TVLI ilipata ruzuku kutoka Serikalini kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kujenga maabara ya kudhibiti ubora wa chanjo. 

Maabara hiyo imeshakamilika na kuanza kutumika. Taasisi ya TVLI inatengeneza makundi ya aina mbili (2) za chanjo: kundi la kwanza ni chanjo dhidi ya bakteria na kundi la pili ni chanjo dhidi ya virusi ambazo zote ubora wake huthibitishwa katika maabara hii.

Kwa kutambua umuhimu wa chanjo ya mifugo na kuongezeka kwa idadi ya chanjo zinazozalishwa ili kuthibitisha ubora wake, kabla ya kuzipeleka kwa wakulima, COSTECH ilitoa ruzuku iliyofanikisha ujenzi wa maabara inayosaidia kupata chanjo zenye ubora.

Kwa sasa maabara imekamilika ina vifaa vyote muhimu vya kupima na kuthibitisha ubora wa chanjo pamoja na uteketezaji wa uchafu utakaozalishwa na maabara (laboratory waste). Hii imeongeza tija katika vipimo vya chanjo kwa kuzingatia ubora kabla hazijapelekwa kwa wafugaji pamoja na wadau wengine wenye uhitaji huo.

Meneja wa kituo, Dkt Stella Bitanyi anasema TVLI ipo kwenye mazungumzo ya kupima ubora wa chanjo zitakazozalishwa na viwanda binafsi wakianza na kiwanda cha Hester Biosciences International kinachoendelea kujengwa mjini Kibaha.

Uwepo wa maabara hii umechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa chanjo kutoka aina tatu (3) zilizokuwa zinazalishwa kabla ya maabara hii mpaka kufikia aina sita (6) ambazo ni chanjo ya: Mdondo wa kuku, Kimeta, Chambavu, Homa ya mapafu ya Ng’ombe, Mchanganyiko (Kimeta na Chambavu) pamoja na Ugonjwa wa kutupa mimba kwa ng’ombe.

Vilevile mradi huu umesaidia kuongeza tija na ufanisi kwa wafanyakazi, wakulima, wazalishaji na waagizaji wa chanjo nchini, hatimaye kukuza pato la Taifa, kuimariisha afya (lishe bora) na kuongeza wigo wa biashara.

 

No comments :

Post a Comment