Wednesday, December 30, 2020

CHUO CHA NIT CHAZINDUA MTAALA WA KOZI YA UENDESHAJI MAGARI NDANI YA VIWANJA VYA NDEGE


Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere(JNIA), Paulo Rwegasha wapili kutoka Kulia akikata utepe kuashiria kuzindua Mtaala wa kozi utoaji wa huduma za uendeshaji magari ndani ya viwanja vya ndege (Airport Vehicle Driving and Operation) jijini  Dar es Salaam leo.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere(JNIA), Paulo Rwegasha wtatu kutoka Kulia akiwa na viongozi wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakionesha mtaala mpya wa kozi utoaji wa huduma za uendeshaji magari ndani ya viwanja vya ndege (Airport Vehicle Driving and Operation) jijini  Dar es Salaam leo baada ya kuuzindua.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere(JNIA), Paulo Rwegasha akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa  uzindua wa Mtaala wa kozi utoaji wa huduma za uendeshaji magari ndani ya viwanja vya ndege (Airport Vehicle Driving and Operation).
Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zacharia Mganilwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtaala wa kozi  utoaji wa huduma za uendeshaji magari ndani ya viwanja vya ndege (Airport Vehicle Driving and Operation) jijini Dar es Salaam leo.

CHUO cha taifa cha Usafirishaji (NIT) kimezindua Mtaala wa kozi  utoaji wa

huduma za uendeshaji magari ndani ya viwanja vya ndege (Airport Vehicle Driving and Operation) ambayo itafungua milango mwingine kwa kuwajengea uwezo wataalamu na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA), Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere(JNIA), Paulo Rwegasha Amesema kuwa mtaala wa kozi mpya umezinduliwa kwaajili ya kusaidia  utoaji huduma ya chakula pamoja na Masuala mazima ya Usafirishaji katika viwanja vya ndege hapa nchini ili kupunguza uhaba wa wataalamu ambapo mtu anaweza kuacha kazi akitegemea hakuna mtu mwenye ujuzi alionao.

Amesema kuwa kigezo kikubwa cha mtu anayetaka kuomba kozi ya 'Airport Vehicle Driving and Operation' yaani mafunzo maalumu ya madereva kwenye viwanja vya ndege anatakiwa kuwa na vigezo vichache ambavyo ni Kuwa na Leseni ya daraja C, D na F ingawa sekta ya usafiri wa anga ikiwa ni pana sana.

"Wanafunzi watakao soma kozi hii watatakiwa kuwa na leseni daraja C, D na F na mfunzo hayo yatafundishwa kwa wiki 10 ambazo ni sawa na miezi miwili na wiki mbili tuu na wataalamu watakuwa wameiva kwaajili ya kusaidia huduma za usafirishaji wa mitambo pamoja na masuala ya ugavi katika viwanja vyetu vya ndege hapa nchini." Amesema Rwegasha.

Hata hivyo amesema kozi hiyo imelenga zaidi katika kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya Usafirishaji hapa nchini.

"Kwa kipindi kirefu sekta ya anga nchini imekuwa katika changamoto ya upungufu wa wataalam mbalimbali na hivyo kukwamisha jitihada mbalimbali za nchi kufikia malengo yake ya kujiletea maendeleo kupitia sekta hii ya usafirishaji." Amesema Regasha.

Licha ya hilo amesema kuwa kutolewa kwa mafunzo hayo na chuo hicho ni hatua kubwa kwa Taifa hususani kipindi hiki ambacho Serikali ya awamu ya tano imeonyesha mwanga mkubwa katika kuiinua sekta ya anga hapa nchini huku kukiwa na mwendelezo wa Ujenzi wa Viwanja vya ndege katika mikoa mbalimbali na manunuzi ya ndege yanaendelea.

Rwegasha amewapongeza niwapongeze Chuo cha taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ubunifu huu wa uzinduzi wa kozi ya umahili wa utoaji ya huduma katika viwanja vya Ndege, hii ni hatua kubwa inayopaswa kupongezwa kwani inazidi kuinua sekta ya anga hapa nchini.

Aidha aliitaka NIT kuendelea kuwa mfano dhidi ya nchi zingine za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma bora na zaidi kijikite kwa kutoa kozi nyingi ili kukiwezesha kutoa wataalam mbalimbali watakasaidia maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zacharia Mganilwa amesema kuzinduliwa mtaala huo ni muendelezo wa jitihada za Chuo cha NIT katika kufanikisha malengo maalumu ya utekelezaji wa mipango ya chuo hicho kuiinua sekta ya Usafirishaji.

 

No comments :

Post a Comment