Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amewataka
Mawaziri na Manaibu Mawaziri kwenda kuchapa kazi huku akiwasisitiza
kufanya maamuzi yanayohusu maslahi ya nchi.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Disemba 9,2020 Ikulu Chamwino
Dodoma wakati akiwaapisha Mawaziri 21 na Manaibu Mawaziri 22 aliowateua
Disemba 5,2020.
"Mkachape
kazi kweli kweli. Nawaomba mawaziri na naibu mawaziri mkafanye maamuzi,
ni nafuu ukafanye uamuzi mbaya kuliko kutokufanya uamuzi kwa sababu
tatizo letu jingine tulilonalo unashindwa kutoa uamuzi kwa sababu hutaki
kuonekana mbaya",amesema Rais Magufuli.
Kafanyeni
uamuzi hasa unaohusu maslahi ya taifa, uamuzi utakaosaidia kuondoa
shida ya wanyonge waliopo vijijini na mimi naamini nimechagua watu wote
watakaokwenda kufanya maamuzi",amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli pia amewataka watendaji wa serikali kutumia vizuri mitandao ya
kijamii na kuepuka kutuma nyaraka za serikali kwenye magroup
'Whatsapp'
"Fanyeni kazi kwa
uadilifu na mkazingatie maadili. Hii teknolojia mpya mkaitumie
vizuri,muache kutumia nyaraka za serikali kwenye magroup",amesema.
No comments :
Post a Comment