Na Jonas Kamaleki - MAELEZO
Miaka 59 ya Uhuru na 58 ya Jamhuri ni kipindi kirefu ambacho mabadiliko makubwa yameonekana yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa ujumla.
Wakati Tanganyika inapata mwaka 1961, wahandisi wazalendo walikuwa
wawili (2), kwa sasa Tanzania ina waandisi walisajiliwa na Bodi ya
Usajili ya Wakandarasi (ERB) zaidi ya 19, 164 hii ikiakisi mabadiliko
maridhawa katika sekta hiyo.
Makandarasi hawa wanaifanya nchi iwe na wataalaam wanaosimamia miradi
mikubwa ya maendeleo ikiwemo ule wa ufuaji wa umeme wa Bwawa la Julius
Nyerere ulioko Rufiji, mkoani Pwani, Ujenzi wa Reli ya kisasa yenye
viwango vya kimataifa (SGR) na miradi mikubwa ya barabara, madaraja,
hospitali na majengo.
Aidha, wakati Tanganyika inapata uhuru, walikuwepo wakandarasi wazawa
wawili (2), mika 59 baadae nchi hii ina wakandarasi waliosajiliwa na
Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) zaidi ya 9,350. Hii inadhihirisha
kuwa nchi imepiga hatua katika eneo hilo ambalo ni jambo la kujivunia.
Ikumbukwe kuwa ili Taifa liweze kuendelea vipo vitu muhimu takriban
vinne, Siasa Safi na Uongozi bora, Ardhi na watu. Watu ndio nguvukazi,
ndio soko la bidhaa, hivyo nchi yenye idadi kubwa ya watu, pamoja vitu
vingine ina uhakika wa nguvu kazi na soko la uhakika la ndani.
Tanganyika ilipopata uhuru kulikuwepo takriban watu milioni 9 na miaka
59 baada ya uhuru, nchi hii ina zaidi ya watu milioni 55.
Maendeleo hayo yamejidhihirisha pia katika nyanja ya Elimu, Afya na
Miundombinu. Wakati Tanganyika inapata uhuru barabara za lami zilikuwa
kilometa 360 tu wakati hivi sasa ni zaidi ya kilometa 14,000. Kipindi
hicho barabara za lami ilikuwa ni kipande cha Dar es Salaam hadi
Morogoro, Tanga- Korogwe na Arusha- Moshi.
Zaidi ya hayo Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na makimbilio ya
nchi jirani ambazo zimekuwa zikikumbwa na machafuko ya kisiasa na
kikabila. Amani hii lazima ilindwe kwani ni mtaji wa maendeleo.
Miaka 59 ya Uhuru na 58 ya Jamhuri itumike kwa watanzania kufanya kazi
kwa bidii ili kujitegemea kiuchumi sawa na Kaulimbiu ya maadhimisho ya
Uhuru mwaka huu isemayo “MIAKA 59 MIAKA 58 YA JAMHURI TANZANIA YENYE
UCHUMI IMARA ITAJENGWA NA WATANZANIA WENYEWE, TUFANYE KAZI KWA BIDII,
UWAJIBIKAJI NA UADILIFU”.
No comments :
Post a Comment