Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapunguzia adhabu wafungwa 256
waliohukumiwa kunyongwa ambapo amesema sasa wapewe kifungo cha maisha.
Rais
Magufuli ametoa msamaha huo leo Disemba 9,2020 ikiwa ni siku ya
kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika wakati akiwaapisha Mawaziri
na Manaibu Waziri aliowateua Disemba 5,2020.
"Kati ya hawa 256 wapo waliohukumiwa kunyongwa kwa sababu ya kuua. Nimeshindwa kuwaua naomba mnisamehe kwa hilo",amesema Rais Magufuli.
"Pia Wafungwa 3316 wa makosa mbalimbali wapunguziwe adhabu na wengine kusamehewa",ameongeza
No comments :
Post a Comment