Rais Dk. John Pombe Magufuli
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema
atafanya uteuzi wa naibu waziri mwingine wa Madini baada ya aliyemteua,
Francis Ndulane Kumba ambaye ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini kushindwa
kuapa leo Jumatano Desemba 9, 2020 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Ndulane
ambaye ni mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) mwenye elimu ya shahada ya
uzamili alikuwa mmoja wa waliotakiwa kuapa lakini ameshindwa kusoma
kiapo mbele ya Rais Magufuli, akikosea mara kadhaa kila alipopewa nafasi
ya kurudia kusoma na ndipo katibu mkuu kiongozi, John Kijazi kumtaka
aende kuketi kwanza ili wenzake waendelee kuapa.
"Kila mmoja nimemuangalia mpaka wewe uliyeshindwa kuapa.
Tutamteua mtu mwingine anayeweza kuapa vizuri",amesema Rais Magufuli.
Kwa
mujibu wa tovuti ya Bunge, Ndulane ana elimu ya shahada ya uzamili
katika uhasibu na fedha ambayo ameisomea katika Chuo Kikuu cha Mzumbe
kati ya mwaka 2013 na 2015. Pia, ana stashahada ya juu ya uhasibu kutoka
Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM).
Ndulani
alisoma shule ya msingi Uwanjani (mwaka 1980 - 1986), baadaye akaenda
sekondari ya Tambaza (mwaka 1987 - 1990) na baada ya kuhitimu kidato cha
nne, alikwenda sekondari ya Pugu (mwaka 1991 - 1993).
No comments :
Post a Comment