Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemuagiza
Waziri wa Ofisi ya Rais -Tamisemi, Suleiman Jaffo kumsimamisha kazi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinary
kutokana na matumizi mabaya ya fedha za Serikali Sh Milioni 400
zilizolenga kuhudumia wananchi lakini akanunua gari la kutembelea.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano wakati akiwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu Chamwino Dodoma.
“TAMISEMI
kuna matumizi mabaya ya fedha Jafo Suleiman Waziri wa TAMISEMI
umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha bado, nimefikiria
sana kukurudisha au kutokukurudisha",amesema Rais Magufuli.
"Hapo
nataka kusema ukweli tuelewane hili la matumizi mabaya. Unakuta
mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 fedha tumehangaika nazo kuzipata
wananchi, watoto wanachangishwa unakuta madawa hayatoshi. Nataka kazi
yako ya kwanza kwenda kumsimamisha mkurugenzi wa Geita ndiyo kazi yako
ya kwanza ukaanze nayo", amesema
No comments :
Post a Comment