Saturday, December 12, 2020

NMB Yatangaza washindi 40 wa DROO ya PILI Mastabata Siyo Kikawaida


Meneja  Mwandamizi Idara ya biashara za Kadi wa Benki ya NMB - Manfred Kayala (katikati) akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya pili ya Promosheni ya Mastabata IsiyoKikawaida iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha uzalishaji Kadi wa Benki ya NMB -Sophia Mwamwitu na kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha - Rasuli Masudi
Meneja  Mwandamizi Idara ya biashara za kadi wa Benki ya NMB - Manfred Kayala akichezesha droo ya pili ya Promosheni ya Mastabata Isiyo Kikawaida  iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha uzalishaji Kadi wa Benki ya NMB-Sophia Mwamwitu na kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha-Rasuli Masudi

  Benki ya NMB imetangaza washindi 40 wa Sh. 100,000 kila mmoja wa droo ya pili ya

Kampeni ya NMB MastaBata Siyo Kikawaida, inayochagiza matumizi ya Kadi za NMB Mastercard na Mastercard QR miongoni mwa wateja wa Benki hiyo. Miongoni mwa washindi ni; Samwel Kilua, Mgonja Tumaini, Msindai Wazael, Saria Fulgence, Joachim Mabula na Alex Katanda.

Kampeni hii ya miezi mitatu ilizinduliwa Novemba 24 mwaka huu, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo za pesa , simu janja ‘smartphone’, jokofu, runinga pamoja na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.

Droo ya pili ya kampeni, imefanyika Makao Makuu ya NMB, jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Rasuli Masudi, aliyewahakishia washiriki na washindi mchakato unaozingatia sheria zote kuwapata.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara za Kadi wa NMB, Manfredy Kayala, alisema katika kipindi chote cha kampeni hiyo, watakabidhi zawadi kwa jumla ya washindi 40 watakaojishindia fedha taslimu 100,000 kila wiki.

Pia, alifafanua kuwa NMB MastaBata itawazawadia washindi 15 simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Sh. 2,480,000 kila mwezi, pamoja na zawadi kuu itakayotolewa katika fainali ya kuhitimisha kampeni hiyo.

"Zawadi kubwa kwenye kampeni hii ni ile ya washindi 15 pamoja na wenza wao kushinda safari ya utalii wa ndani iliyolipiwa kila kitu na NMB, ambapo mshindi na mwenza wake watapata nafasi ya kutembelea Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.

"Aidha, washindi wa fainali watawapa ruksa ya kuchagua utalii wa ndani au kuchukua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu la Milango Miwili, Kompyuta Mpakato, Simu Janja (Samsung A70), Water Dispenser na Microwave," alisema Kayala

Kwa upande wake, Masudi kutoka GBT, aliwatoa shaka wateja wa NMB wanaoshiriki kampeni ya NMB Mastabata Siyo akisema mchakato wa kutafuta na kutangaza washindi, unafanyika kisheria chini ya bodi hiyo na kwamba hakuna ubabaishaji katika hilo.

Aliwataka wateja  wa NMB waendelee kufanya manunuzi kutumia kadi za NMB Mastercard, Mastercard QR, pamoja na POS ili kushiriki kinyang'anyiro hicho mara nyingi wawezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi za wiki, mwezi na hata 'grand finale' Februari 2021.

No comments :

Post a Comment