MKURUGENZI wa kampuni ya Mr. kuku farmer ltd, Tariq Machibya (29), maarufu kama Mr Kuku, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kufanya biashara haramu ya upatu na kukusanya fedha za umma sh. Bilioni 17, amehukumiwa kulipa fidia ya zaidi y sh. Bilioni 5.4 baada ya kukiri mashtaka ya kushiriki katika upatu na kupokea miamala ya fedha kutoka kwa umma.
Pia
mahakama imemuhukumu mshtakiwa kulipa faini ya sh. Milioni tano ama
akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.
Aidha
mahakama imeamuru fedha sh. 5,456,480.41 ambazo zipo katika akaunti za
mshtakiwa zitaifishwe na kuwa mali ya serikali. Na pia mahakama imeamuru
fedha hizo kuhamishiwa katika akaunti namba 9921169817 iliyoko Benki
Kuu ya Tanzania kwa jina la Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi amesema mahakama imezingatia kwamba mshtakiwa amekiri
mwenyewe makosa yake na ni mkosaji wa mara ya kwanza na wameangalia
makubaliano hivyo hakuna sababu ya kumpa adhabu kali
Mapema,
Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai leo Desemba 16, 2020 mshitakiwa pamoja
na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) wameingia makubaliano , katika
mashtaka saba aliyokuwa anakabiliwa nayo yameondolewa na wamebakisha
mashtaka mawili
Akisomewa mashtaka hayo mawili, katika shtaka la
kusimamia biashara ya upatu inadaiwa kati ya Januari 2018 na Mei, mwaka
huu, maeneo tofauti Dar ea Salaam alijihusisha na biashara hiyo kwa
kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma kwa kujifanya watafanya
ujasiriamali wa ufugaji kuku na watapata faida asilimia 70 ya mtaji wa
awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa uwekezaji
wa miezi sita kiasi ambacho ni kikubwa kibiashara kuliko mtaji
uliokusanywa.
Pia katika shtaka la pili mshtakiwa anadaiwa kukubali kupokea muamala wa kifedha kutoka kwa umma kiasi cha Sh bilioni 17
Awali
mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka saba ambapo mbali na hayo
mawili yalikuwepo mashtaka matano ya utakatishaji fedha.
Kabla
ya kusomwa kwa adhabu, Wakili Kadushi aliieleza mahakama kuwa, hawana
kumbukumbu za makosa ya nyuma ya washitakiwa hivyo, ameiomba mahakama
kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria huku ikizingatia hatua ya
makubaliano waliyofikia.
Hata hivyo, wakili wa Utetezi, Augustine
Shio ameiomba mahakama impunguzie mshtakiwa adhabu kwani amekiri
makosa yake mwenyewe na pia ana familia ya wake wa watatu ambao kila
mmoja anamtoto mchanga na wote wanamtegemea yeye, pia Wakili Shio
ameiomba mahakama ifikirie kumpa mshtakiwa adhabu nyeusi isiyokuwa na
faini kwani alipokamatwa fedha zake zote zilipokamatwa na zimetaifishwa
na serikali hivyo naomba apewe adhabu ambayo ataweza kuitekeleza na
kwenda kujiunga na familia yake.
No comments :
Post a Comment