Meneja wa Udhamini na
Matukio wa Benki ya CRDB , Lilian Kanora katika mkutano wa waandishi wa habari wakati wa
kutangaza washindi wa kampeni ya JIPE 5 na Scholar ambayo inaendeshwa na Benki
ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo hapa nchini.Sehemu ya zawadi kwa wanafunzi hao.
======= ====== ======
Benki
ya CRDB imetoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini ikiwa ni
sehemu ya kampeni ya JIPE 5 ambayo ilizinduliwa mwezi Oktoba mwaka huu
ikiwa na malengo ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba kuelekea
mwisho wa mwaka.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja Mwandamizi wa Idara ya
Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Abel Lasway amesema kuwa hadi kufikia
tarehe 16 mwezi huu, benki tayari imeshatoa jumla ya zawadi zinazofikia
Shilingi Mlioni 20. Zawadi hiyo zimetolewa kwa wateja zaidi ya 4000 huku
akaunti zaidi ya 74,000 zikiwa zimekwisha funguliwa.
“Tunawashukuru
sana Watanzania kwa kuipokea vyema kampeni ya Jipe Tano ambapo
mafanikio yaliyopatikana sio tu ni kwa faida ya Benki ya CRDB bali
yanaonyesha ni kwa jinsi gani Benki ya CRDB imeweza kuwajumuisha
Watanzania wengi katika mfumo rasmi wa huduma za fedha,” alisema Lasway.
Meneja
huyo mwandamizi alisema katika kampeni hiyo ya Jipe Tano makundi
mbalimbali ya wateja yameweza kuzawadiwa ambapo kwa mwezi huu wa Disemba
Benki inawazawadia ada za shule wazazi wanaofungua akaunti ya watoto za
Junior Jumbo. Jumla ya Shilingi Milioni 30 zimeandaliwa kwa ajili ya
kutolewa kama zawadi ya ada kwa akaunti za watoto za Junior Jumbo
zitakazofunguliwa mwezi Disemba.
“Benki
ya CRDB tunajinasibu kwa kauli mbiu yetu ya “Ulipo Tupo” ambayo
haiishii tu kufikisha huduma mahali ambapo wateja wetu wapo bali
inalenga kuhakikisha Benki inakua pamoja na mteja katika hatua zote za
maisha yake,” aliongezea Lasway.
Sambamba
na zawadi hizo kwa akaunti za akiba na watoto, alisema Benki ya CRDB
pia ililenga kundi la wanafunzi wa vyuo ambavyo vimefunguliwa hivi
karibuni ambapo timu ya mauzo ya Benki iliweka kambi katika vyuo
mbalimbali nchini ili kutoa elimu ya masuala ya fedha pamoja na kutoa
huduma za kufungua akaunti kwa wanafunzi.
“Nimefurahi
kuona tumeweza kufanikiwa kuwaingiza katika mfumo rasmi wa fedha
wanafunzi wengi na tukaona pamoja na kuwapa huduma hizi tuweze
kuwazawadia vitu ambavyo vitarahisha maisha yao wawapo chuoni,” alisema
Lasway huku akiongeza kuwa kupitia kampeni hiyo ya wanafunzi ya JIPE 5
na Scholar, jumla ya wanafunzi 100 kutoka vyuo mbalimbali nchini
watazawadiwa laptop (kompyuta pakato) na smart phone (simu janja).
No comments :
Post a Comment