Friday, December 4, 2020

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi awataka madiwani kuboresha maisha ya wananchi.

 Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa(NEC) Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya Arusha Dc. (Picha na Jane Edward, Arusha).

 Na Jane Edward Michuzi TV, Arusha

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC)Wilson Mahera amewataka madiwani ya halmashauri ya Arusha DC  kuhakikisha wanaboresha maisha ya

wananchi wao  kwa kuleta maendeleo .

Aliyasema hayo leo wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha kuapishwa kwa madiwani hao kilichofanyika katika halmashauri hiyo.

Mahera alisema kuwa,wananchi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo matarajio yao ni kutatuliwa na madiwani hao ambao ndio wawakilishi ,hivyo aliwataka kuwa watatuzi wa changamoto na migogoro katika kata hizo na sio kuwa chanzo cha migogoro.

Naye Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi ,Noah Lembris aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kufuata taratibu na kanuni zilizopo katika halmashauri hiyo huku wakiepukana na tamaa mbaya ya kupokea rushwa ambayo mwisho wa siku itawapelekea kushindwa kutoa huduma kwa wananchi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha DC,Saad Mtambulo aliwataka madiwani hao  kufuata sheria na kanuni za halmashauri hiyo huku wakihakikisha wanawatumikia wananchi kwa haki sawa bila ubaguzi wowote.

Nao Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo ,Diwani wa kata ya Bangata,  Ezra Tomito alisema kuwa, kazi imeanza ya kuwatumikia wananchi na kuwa watahakikisha wanatatua changamoto mbalimbali katika kata zao huku wakianza na vipaumbele alivyojiwekea ikiwemo barabara,maji na elimu.

Diwani  pekee wa kike katika Jimbo  la Arumeru Magharibi katika kata ya Moivo , Selina Mollel alisema kuwa,wananchi wanatakiwa kutambua kuwa ndo neema imeanza na kuwa anaenda kufanya kazi rasmi na kutatua kilio cha wananchi wake kwa kuanza na vipaumbele mbalimbali.

 

No comments :

Post a Comment