Friday, December 4, 2020

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI DAR, JUKWAA LA WAHARIRI WALAANI VIKALI KITENDO KILICHOFANYWA NA MKURUGENZI WA TEMEKE


Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania,  Deodatus Balile akizungumza na waandishi wa habari kulaani kitendo cha  udhalilishwaji alichofanyiwa Muandishi wa ITV nchini, Richard Steven na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Lusubilo Mwakabibi.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania,  Deodatus Balile akizungumza na waandishi wa habari kulaani kitendo cha  udhalilishwaji alichofanyiwa Muandishi wa ITV nchini, Richard Steven na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Lusubilo Mwakabibi, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dar es Salaam Irene Meero.

Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dar es Salaam Irene Meero, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tamko dhidi ya kitendo cha udhalilishwaji alichofanyiwa Muandishi wa habari wa  ITV, Richard steven na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi mapema wiki hiii jijini Dar es Salaam

 CHAMA cha waandishi wa habari Mkoa wa Dar es salaam (DCPC)kwa kushirikiana na Jukwaa la

Wahariri  (TEF) limelaani vikali  kitendo kilichofanywa na Mkurungezi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi  dhidi ya Mwandishi wa Habari wa kituo cha ITV Richard Steven  ma kukiitia kitendo hicho ni udhalilishaji mkubwa.

Akitoa tamko dhidi ya kauli alizotoa Mkurugenzi huyo,   Mwenyekiti DCPC Irene Meero amesema Mkurungezi huyo amefanya udhalilishaji mkubwa si tu kwa Mwandishi huyo  pekee bali  ni kwa tasnia nzima ya habari Nchini.

Akielezea chanzo cha yote hayo, Irene amesema mwanzoni mwa wiki hii Steven alimpigia simu Mkurungezi Mwakabibi kuomba kwenda ofisini kwake kupata ufafanuzi juu ya kuwepo kwa hali ya sitofahamu kati ya wananchi wa mtaa wa magogoni, Yombo Dovya baada ya Manispaa hiyo kuanza ujenzi wa shule ya sekondari Lumo.

Irene amesema kutokana na sitofahamu hiyo wananchi wa eneo hilo, walijitokeza kuzuia ujenzi huo na kudai kuwa  eneo hilo linamgogoro ambao bado upo mahakamani .

Amefafanua kuwa, kufuatia hali hiyo, baadhi ya vyombo vya habari vilivyokuwepo katika eneo la tukio viliwahoji maofisa wa serikali waliokuwepo ambao walisema mtu pekee mwenyewe Mamlaka ya kuzungumza kadhia hiyo ni Mkurungezi wa Manispaa , ndipo Mwandishi huyo wa ITV alipompigia Mkurugenzi huyo na kuomba kwenda ofisini kwake kwa ajili ya kupata ufafanuzi.

Hata hivyo baada ya kupiga simu Mkurungezi alipokea Simu na muandishi kumueleza shuda take, alianza kutoa kauli za kejeli na dhiaka" wewe ni nani unaweza kupiga simu? Unasema unataka kuja kuniona? wewe ni Nani? .

Irene amesema hata baada ya maswali hayo Mwandishi alirudia kujitambulisha pamoja na kumnyenyekea kwa kurudia kuomba kumuona lakini Mkurungezi  aliendelea kutoa kauli iliyosheheni kiburi na kumtaka Mwandishi kujipima kama ana hadhi ya kukutana nae na kumtaka amwambie Mkurungezi wake(ITV) ndiye ampigie simu kwa vile yeye sio 'level yake'.

" Kitendo cha Mkurugenzi huyo kukataa kutoa ushirikiako kwa wanahabari ni kuvunja sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 kifungu cha 7 ambacho kinampa Mwandishi Mamlaka ya kukusanya, kuchakata na kuchapisha habari"amesema

Alifanunua zaidi kitendo kilichofanywa na Mkurungezi huyo si tu kwamba athamini haki ya waandishi kupata habari katika Manispaa yake bali pia atambui wajibu na haki za tasnia ya habari katika kuwajengea imani na serikali yao .

Aidha DCPC na TEF wamemtaka Mwakabibi kumuomba radhi Mwandishi huyo na tasnia ya habari kwa ujumla.

Naye, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile awataka viongozi kutambua umuhimu wa vyombo vya habari sambamba na kuwaheshimu waandishi wa habari.

Hata hivyo Balike amewataka ya waandishi wa habari nchini kuendelea na majukumu yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kwenda kuchukua habari katika Manispaa ya Temeke hata kama ni kumuhoji Mkurugenzi huyo..

"Mkurungezi wa Manispaa ya Temeke anapaswa kutambua kuwa kazi hizi zinafanana hakuna kazi nzuri iliyo bora kuliko yake na hatutamfungia mtu kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki wananchi wa Manispaa ya Temeke"amesema Balile

 

 

No comments :

Post a Comment