***********************************************
23,des
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKOA wa Pwani
,umepiga hatua kali na kufikia kuwa na viwanda vikubwa,vya kati,vidogo
na vidogodogo 1,236 kwa mwaka 2020 kutoka viwanda 396 kwa mwaka 2016.
Kasi hiyo ya ujenzi
wa viwanda ni kubwa ndani ya miaka minne ,ambapo viongozi watendaji wa
mkoa huo wameamua kuongeza jitihada za kuhamasisha wawekezaji ili
kuhakikisha mkoa huo unakuwa UKANDA WA VIWANDA.
Akielezea mafanikio
hayo ,mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,bado
wamejipanga kuongeza viwanda na wawekezaji ili kutekeleza ilani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Pamoja na hayo
,alieleza kati ya wilaya zote mkoani hapo ,lakini bado wilaya tatu ya
Kibiti,Rufiji na Mafia zinasuasua kufikia kasi hiyo .
Kutokana na hilo ,ameelekeza nguvu ielekezwe katika wilaya hizo kwani fursa zipo .
“Tunapokea pongezi na
sifa nyingi kutoka kwa viongozi wakuu Taifa akiwemo Rais John Magufuli
,mikoani na nchi mbalimbali hivyo nawataka viongozi mkoa kuendelea
kulinda maendeleo hayo na kuinua sekta ya viwanda” alibainisha Ndikilo.
Akielezea juu ya
sekta ya elimu ,ameelekeza kuhakikisha madarasa yanayopaswa kujengwa
yajengwe ,ili wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
January 2021 wawe wote darasani ,kwani bado wanafunzi 6,577 wanaonekana
watakosa kuingia madarasani.
Akizungumzia tatizo la upungufu wa watumishi , alisema pamoja na juhudi za mkoa lakini changamoto hii inajirudia kila mwaka.
Katibu tawala
msaidizi mipango na uratibu Edward Mwakipesile alifafanua ,kuna
changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi mbalimbali na idara ya afya
upande wa wataalamu wa Xray ni shida .
Nae mkuu wa wilaya wa Mafia , Shaibu Nnduma alisema ,idara 14 zinakaimisha watendaji na wote wanaokaimu hawana sifa.
Kufuatia changamoto
hiyo ,katibu mkuu TAMISEMI alifikishiwa taarifa hizo na kuomba tena
awasilishiwe juu ya hilo na kuhusiana na tatizo la Mafia amedai atafika
mwenyewe Mafia .
No comments :
Post a Comment