Thursday, December 3, 2020

MDEE, BULAYA NA KISHOA WAMTAMBULISHA WAKILI MPYA

WABUNGE wa viti maalumu (Chadema), Halima Mdee, Ester Bulaya na Jesca Kishoa, wamemtambulisha wakili mpya atakayewatetea katika kesi yao ya

mashtaka saba likiwemo la kufanya mkusanyiko na kutotii amri halali katika gereza la Segerea.

Wabunge hao ambao hivi karibuni walitangazwa kuvuliwa uanachama wa chama chao cha Chadema leo Desemba 3, 2020 wamefika katika mahakama ya Hakimu Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kesi ya kusomewa maelezo ya awali, wamewakilishwa na wakili Emmanuel Vkandis

Wabunge hao wanashtakiwa mahakamani hapo na wenzao 24 ambao wote kwa pamoja wanatetewa na wakili Peter Kibatala.

Awali washtakiwa hao wote walikuwa wakitetewa na wakili Hekima Mwasipo.

Washtakiwa hao wanaotetewa na Kibatala ni, Boniface Jakobo, Patrick Assenga, Henry Kilewo,Yohana Kaunya, Kedmony Mhembo, Mshewa Karua, Khadija Mwago, Pendo Raphael maarufu kama Mwasomola na mkazi wa Bonyokwa, Cesilia Michael, Happy Abdalla; Stephen Kitomali  na Paul Makali.

Hata hivyo mahakama imeshindwa kuwasomea washtakiwa hao PH na badala yake imetoa hati ya kukamatwa kwa washitakiwa wawili, Edgar Adelini, Reginald Masawe, ambao hawajafika mahakamani hapo leo bila taarifa yoyote. 

Mapema wakili wa serikali Ester Martin alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo leo imeitwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali lakini washtakiwa wawili hawajafika hivyo wameomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo hayo na pia wameomba hati ya kukamatwa kwa washtakiwa hao.

Katika hatua nyingine, mdhamini wa mshtakiwa Kedmony Mhembo, Remigius Bafuluki amewasilisha ombi la kujiondoa kumdhamini mshtakiwa huyo, lakini Hakimu amemwambia atajitoa pale ambapo atapatikana mdhanimi mwingine na amemtaka mshtakiwa Mhembo kutafuta mdhamini mwingine.

Kati ya mashtaka hayo saba yanayowakabili, matatu ni ya kutoa lugha ya kuudhi yanayowakabili, Mdee, Bulaya na Jacob; moja ni kuharibu Mali; kufanya mkusanyiko usio kuwa wa halali; kutotii amri halali iliyowekwa na Jeshi la Magereza na shambulio

Inadaiwa, Machi 13, 2020 , eneo la gereza la Segerea, lililopo wilaya ya Ilala, kwa makusudi washtakiwa walikaidi amri halali ya kuondoka eneo la gereza kwa amani ili eneo hilo libaki wazi, amri hiyo iliyotolewa na askari mwenye namba B 3648, Sajenti John ambaye ni mlinzi wa Geti la gereza hilo.

Katika shtaka pili ambalo ni la kufanya mkusanyiko,  washtakiwa wanadaiwa kukusanyika  isivyo halali kwenye geti la Gereza la Segerea na kusababisha hofu iliyokuwa inapelekea uvunjifu wa amani na utulivu.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuharibu geti kuu la kuingilia na kutokea katika gereza la Segerea mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia huku Mdee, Bulaya na Jacob wakidaiwa kutoa lugha ya matusi kwa askari Magereza mwenye namba B 3648, Sajent John.

 Aidha mshtakiwa Jacob pia anadaiwa kumshambulia askari Magereza  Sajente John kwa kumvuta shati na kumchania, wakati akiwa katika utekeleza wa majukumu yake ya ulinzi kwenye geti kuu la gereza la Segerea.

 

No comments :

Post a Comment