WIZARA ya Kilimo kwa kushirikiana na Asasi ya Mazao ya Bustani(TAHA) wameandaa
kongamano kubwa la kikanda kwa lengo la kuongeza hamasa ya uwekezaji na kuibua fursa mpya za biashara ya mazao ya bustani nchini ambayo ni matunda, mbogamboga, maua na viungo.Kongamano
hilo litafanyika Jumamosi ya Desemba 5,2020 katika hoteli ya Hyatt
Regency jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam,Mtendaji Mkuu wa TAHA Jacqueline Mkindi amesema itakumbukwa hivi
karibuni Rais John Magufuli wakati akilihutubia Bunge la 12 Novemba
13,2020 alianisha vipaumbele kadhaa ili kuimarisha sekta ya kilimo cha
mazao ya bustani.
Ametaja baadhi ya vipaumbele hivyo ni kuweka mkazo mkubwa kwenye kilimo cha mazao ya bustani yaani matunda, mbogamboga maua na viungo, katika kuendeleza kilimo cha mazao ya bustani Serikali imekusudia kununua ndege moja ya mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya bustani, minofu ya samaki na nyama, "Rais alizitaka Wizara ya Kilimo, Biashara na Mambo ya Nje , mabalozi na sekta binafsi kujipanga katika kutafuta masoko na kusaini makubaliano yatakayonufaisha nchi yetu.
"Kama sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli na ili kuhakikisha uwekezaji na upatikanaji wa masoko ya bidhaa na huduma katika tasnia ya kilimo cha mazao ya bustani zinaongezeka; Wizara ya Kilimo inaungana na TAHA kufanya kongamano hilo kubwa la uwekezaji,"amesema.
Amesisitiza kongamano hilo litaongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kuhakikisha sekta ya kilimo cha mazao ya bustani inaendelea kukua kwa kasi kwa ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi katika kutekeleza vipaumbele vilivyotajwa na Rais Magufuli.
Aidha
amesema uwepo wa kanda ya kibiashara za Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) zenye
idadi ya watu wapatao milioni 500, inaashiria fursa kubwa ya soko la
bidhaa za mazao ya bustani.
"Hii ni fursa kubwa kwa wadau wa
sekta binafsi kwa kushirikiana na Serikali kuwekeza katika mnyororo wa
thamani wa tasnia ya kilimo cha bustani.Kuwekeza katika mnyororo wa
thamani kutafungua fursa mbalimbali za uwekezaji na masoko ya bidhaa za
mazao ya bustani,"amesema.
Amesema TAHA inawataarifu tayari baadhi ya
washiriki wakubwa wataanza kuwasili kuanzia leo mpaka kesho kutoka
Rwanda, Kenya, Sudan, DRC Congo, Comoro na Malawi."Tunatarajia kuwa na
washiriki zaidi ya 400 , wengine zaidi ambao watafuatilia mubashara
kupitia mtandao wa kijamii ya TAHA.
"Naomba kuwaarifu watanzania
ambao ni wazalishaji ,wafanyabiashara, wasafirishaji , wasindikaji na
wadau wengine wakubwa wa horticulture hata kama walishindwa kwa namna
moja au nyingine kujisajili kwa muda uliokuwa umepangwa kuhudhuria
mkutano huu wa aina yake,"amesema Mkindi.
No comments :
Post a Comment