Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MKUU
wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amekemea vikali Bohari ya kuhifadhi
Kemikali ya Junaco Group Ltd kukosa vigezo na kutofuata Sheria na
Taratibu za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Shirika la
Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tina (TMDA) katika
uhafadhi wa Kemikali wa hizo.
DC
Gondwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake eneo la Bohari hiyo iliyopo
Mivinjeni jijini Dar es Salaam, ametoa wito kwa kwa Taasisi hizo
kufuatilia Bohari kama hizo kuhakikisha wanafuata Sheria ili kuwalinda
Wananchi haswa Wakazi wa eneo hilo la Temeke.
“Wafanyabiashara
wa hizi Kemikali kwa kweli hatujui zikikaa vibaya hatuwezi kujua kabisa
kama zimeharibiaka au kutoboko wapi, zinaweza kuleta madhara
Vipindupindu, na maradhi mbalimbali kwa Jamii”, amesema DC Gondwe.
Kwa
upande wake, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali, Gerald Mollel amesema wamegundua mambo ambayo
hayaendani na matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kemikali nchini,
kuchanganya Kemikali hizo sehemu ambazo sio sawa, baadhi ya Kemikali
kuisha muda wa matumizi.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe akielekezwa jambo na Meneja wa Kanda
ya Mashariki, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Gerald
Mollel wakati alipotembelea Bohari ya kuhifadhia Kemikali ya Junaco
Group Ltd, eneo la Mivinjeni, Jijini Dar es salaam leo.
Mollel
amesema kutokana na uwepo wa Bohari hiyo Kemikali hizo zinaweza kuleta
madhara kama kusambaa na kusababisha magonjwa ya Saratani, Vipindupindu
na magonjwa ya tumbo.
Naye
Afisa Mkaguzi Mwandamizi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi
Donald Manyama amekiri kuwepo sehemu kubwa ya Kemikali hizo kupitwa na
wakati (Expired) lakini zinaendelea kuonekana katika sehemu hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe (kushoto) akisisitiza jambo wakati
akitoa maelekezo kwa Afisa wa Bohari ya kuhifadhi Kemikali ya Junaco
Group Ltd, Mbwana Guju juu ya uhifadhi wa Kemikali wakati alipotembelea
Bohari hiyo, eneo la Mivinjeni, Jijini Dar es salaam leo.
“Walipaswa
kufuata taratibu kutengenisha zile zilizoharibika na zile ambazo hazija
haribika na kutoa taarifa mapema kwa Mamlaka zinazo husika na usamamizi
wa Kemikali, Kemikali nyingine tumepeleka Maabara kufanya utafiti
kupata majibu ya haraka”, amesema Manyama.
Mwakilishi
wa Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa
wa Temeke, Joseph Paul amewataka Wafanyabiashara wanaofanya biashara
hizo za Kemikali kufuata na kuzingatia taratibu za nchi ikiwemo kufuata
weledi katika kufanya biashara hizo, amezitaka Mamlaka zinazo fanya
ukaguzi kuongeza kasi ya ukaguzi.
No comments :
Post a Comment