Friday, December 4, 2020

DKT.MSUYA AFUNGUKA NAMNA CHUO CHA UDOM KINAVYOKUZA KIWANGO CHA MAADILI PAMOJA NA KUPAMBANA NA RUSHWA YA NGONO


Afisa Uhusiano wa TAKUKURU Doreen Kapwani,akitoa elimu kwa waandishi wa habari jijini Dodoma jinsi ya kuandika  kwa ufasaha bila kupotosha habari kuhusu Utafiti wa Rushwa ya Ngono uliofanywa na taasisi hiyo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Mkurugenzi Uzuaiji Rushwa TAKUKURU Bi.Sabina Seja,akizungumza kwenye kikao cha waandishi wa habari na Viongozi wa TAKUKURU

Afisa wa TAKUKURU Bw.Juwenary John ,akitoa utafiti kwa waandishi wa habari jijini Dodoma walioufanya kuhusu Rushwa ya Ngono katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt.Ombeni Msuya,akielezea mikakati mbalimbali iliyowekwa chuoni hapo kupambana na Rushwa ya Ngono.

Mkurugenzi Taasisi ya Taaluma za Jinsia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Lulu Mahai,akizungumzia  mikakati mbalimbali iliyowekwa chuoni hapo kupambana na Rushwa ya Ngono.

Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina ya mkutano ulioitishwa na TAKUKURU kwa waandishi hao uliofanyika leo   jijini Dodoma.

Mwaandishi wa Gazeti la Daily News Katare Mbashiru akiuliza Swali wakati wa Kikao cha waandishi wa habari na viongozi wa TAKUKURU jijini Dodoma

Mwaandishi wa Gazeti la Habari Leo Magnus Mahenge,akichangia maada wakati wa

Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TAKUKURU mara baada ya kuwapatia Elimu kuhusu masuala ya rushwa ya ngono vyuoni iliyofanyika jijini Dodoma.

……………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

CHUO KIKUU Cha Dodoma (UDOM) kimesema kitaendelea kupambana na changamoto ya rushwa ya ngono wanazokutana nazo wanafunzi wao kwa kukuza kiwango cha maadili kwa watumishi wake pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kupambana na utovu wa maadili.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili chuoni hapo, Dkt Ombeni Msuya ambaye amemuakilisha Makamu Mkuu wa Chuo hiko katika kikao kazi cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi wa utafiti wa rushwa ya ngono uliofanywa na taasisi hiyo.
Akizungumza katika mkutano huo, Dkt Msuya amesema katika kukabiliana na changamoto ya rushwa ya ngono chuoni hapo wameanzisha madawati ya jinsia katika kila Idara zilizopo na kila Idara ikiwa na kiongozi wake jambo ambalo linawafanya wanafunzi wawe na sehemu ya kukimbilia wanapopata changamoto hiyo.
Amesema Chuo Kikuu cha UDOM pia kimeanzisha masanduku ya kutoa maoni kila mahali ndani ya Chuo hiko hasa katika Hosteli, Migahawani lengo likiwa ni kumuwezesha kila anaeona changamoto hiyo au vitendo hivyo vya utoaji rushwa ya ngono basi aweze kutoa taarifa ili taasisi iweze kushughulika nayo.
” Udom ni sehemu ya jamii, hivyo inawezekana wapo watu wachache wenye utovu wa nidhamu lakini wengi wanazingatia maadili. Chuo kinatoa pia elimu na hata jana tulikutana na wanafunzi wa mwaka wa kwanza na kuwajengea uelewa na elimu hii ya rushwa sambamba na kuwaambia umuhimu wa kutoa taarifa wanapopata hizo changamota.
Tumefungua pia madawati ya malalamiko kwenye maeneo mbalimbali ya Chuo chetu hadi kwenye Hospitali yetu lakini pia kuna Klabu ya wapinga rushwa UDOM ambayo ina miaka 10 hadi sasa, klabu hii ina wanafunzi, viongozi na watumishi na imekua msaada mkubwa sana katika kudhibiti na kuzuia vitendo hivi vya rushwa ya ngono,” Amesema Dkt Msuya.

Naye Mkurugenzi wa Tasisi ya huduma za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM Lulu Muhai amesema wamefungua ukusanjaji wa taarifa kwa kuwa na namba ya simu kwa wanafunzi kupiga simu pindi wanapokutana na changamoto ya rushwa ya ngono kwa wahadhiri wao.

Pia amesema wameaajiri wafanyakazi 36 wa jinsia zote wakike na wanaume ambao kazi yao kubwa ni kupokea malalamiko kwa wanafunzi na baadhi ya wafanyakazi,na pia tumeandaa vipeperushi vinavyoelezea uadilifu.

Kwa Upande wake Afisa Takukuru Juwenary John amesema zipo sababu nyingi zinazosababisha kuendelea kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono.

Amesema Katika utafiti uliofanywa katika Taasisi za elimu ya juu vyuo vikuu viwili Chuo Kikuu cha Dar Es salaam (UDSM)na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) sababu zinazosababisha ni pamoja na Mmomonyoko wa maadili,matumizi mabaya ya madalaka,mikakati dhaifu ya kutekeleza sheria za rushwa ya ngono na uelewa hafifu.

“Hii inasababisha waathiriwa wa rushwa ya ngono kuendelea kuumia kimya kimyaa ambapo wakosaji kuendelea na vitendo hivi bila kuchukuliwa hatua stahiki za sheria,”Amesema John.

Amesema ni Tafiti zinabaini kwamba tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo vya elimu ya juu na vilivyoshiriki lipo na tatizo hili ni kubwa na si lakupuuza kwani Shuhuda za waathirika zimetambuliwa.

Aidha amesema rushwa ya ngono hugeuza haki ya muombwaji kuwa upendeleo na sio stahiki kwani inahusu kumpokonya mtu haki yake,kusababisha madhara kwenye nyanja mbalimbali kama vile kupata jelaha lisilo tibika kwenye maisha yake hata pahala pengine.

” Muhanga anaweza kugeuzwa mtumwa wa ngono,hivyo kushindwa kukuza vipaji vyake vya uhalisia ni ukweli usiopingika hali hii huathiri uchumi wa taifa,” amesema Afisa huyo Takukuru John.

 

No comments :

Post a Comment