Friday, December 25, 2020

ASKOFU SANGU AENDESHA IBADA MKESHA KRISMASI....ATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI



TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga, Liberatus Sangu, akiendesha ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya KrismasI, katika Kanisa kuu la Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa salamu za Serikali, kwenye mkesha wa siku kuu ya Krismasi.
 Waumini wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi
Waumini wakiendelea na ibada kwenye mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
Ibada ikiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (wa kwanza kushoto), akiwa na waumini wakiendelea kusali kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
Ibada ikiendelea.
 
Ibada ikiendelea.
Waumini wakitoa sadaka.
Waumini wakiendelea kutoa Sadaka.

Awali Askofu Sangu, akibariki waumini wakati akiingia Kanisani kuendesha Ibada ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.

 Askofu Sangu akibariki waumini kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
Awali Askofu Sangu, akiingia kanisani kuendesha Ibada ya sikukuu ya Krismasi.
Awali Askofu Sangu, akiingia kanisani kuendesha Ibada ya sikukuu ya Krismasi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

 

Askofu wa Kanisa la Roman Katoliki jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu awali akiingia kanisani kwa ajili ya kuendesha  Ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Kristmas.

Na Marco Maduhu, Shinyanga. 

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu, amewataka Watanzania kudumisha amani ya nchi ili waishi kwa upendo, utulivu, na kufanya shughuli za maendeleo.

Askofu Sangu amebainisha hayo jana wakati akiendesha Ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Krismasi, iliyofanyika usiku kwenye Kanisa kuu la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko. 

Alisema watanzania wanapaswa kuilinda amani ya nchi, ambayo iliasisiwa na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kuacha kuichezea ili kutoingia kwenye machafuko. 

“Nawaomba watanzania tuidumishe amani ya nchi yetu, bila amani hakuna upendo, furaha, wala maendeleo, na kuna mataifa yana wivu sana na Tanzania, na kutaka tufarakane ili kuvuruga amani tuliyonayo, tusikubali bali tuilinde na kuidumisha amani ambayo tuliachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,” alisema Sangu. 

Katika hatua nyingine Askofu Sangu aliipongeza Serikali mkoani Shinyanga  kwa kupunguza tatizo la mauaji ya vikongwe, na kuomba kasi iongezwe zaidi kumaliza kabisa mauaji hayo ya watu wasio na hatia, hasa katika maeneo ya vijijini ambapo bado yanaendelea. 

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alimuahidi Askofu Sangu kuwa maombi yake yote ambayo ameyaomba kwa Serikali yatatekelezwa, huku akiwataka wananchi wawe na hofu ya Mungu na kutenda yaliyo mema na kuacha kufanya mambo maovu, pamoja na kusheherekea sikukuu kwa amani na utulivu.

No comments :

Post a Comment