Saturday, November 7, 2020

WAJASIRIAMALI WAPEWA SOMO

Mdau wa maendeleo na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii,Mugabe Kihongosi akizungumza na wanahabari.
………………………………………………………………………………………….
NA DENIS MLOWE,IRINGA

WAJASIRIAMALI wadogo wa mkoa wa Iringa wametakiwa kutoanzisha biashara zao


kwa mihemko na badala yake kufanya utafiti wa kutosha wa aina ya biashara
anayoitaka kuifanya.

Akizungumza na mwanahabari mdau wa maendeleo na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii mkoa wa Iringa, Mugabe Kihongosi alisema kuwa wajasiliamali wengi wanatakiwa kujua udhaifu na uimara wa biashara anayotaka kuianzisha ili kuweza kufanya vyema kuliko kukurupuka katika kuanzisha biashara ambayo mwisho wa siku inakufa bila kufahamu nini chanzo.

Kihongosi alisema wajasiriamali wengi wadogo  wameshindwa kufanikiwa katika biashara zao kwa kushindwa kupata taarifa za kutosha kwa biashara wanazotaka kufanya na badala yake wanaiga biashara inayofanywa na mwingine bila kufanya utafiti hali inayowaghalimu wengi..

Alsema soko la sasa ni la ushindani ni lazima kuwa mbunifu na kutumia madhaifu ya wengine katika kujiimarisha huku akisisitiza kujisomea maandiko tofauti tofauti ili kupata maarifa zaidi juu ya mazingira ya soko la sasa linahitaji nini kwenye biashara.

Alisema kuwa wajasiliamali wengi wamekuwa wakifanya biashara kwa mazoea ili
Hali kwa soko la Sasa linahitaji ubunifu mkubwa katika kufanya biashara ikiwemo kujua aina ya wateja ambao unawahudumia.

Aliongeza kuwa soko lolote duniani linahitaji ubunifu na jinsi dunia ilivyo kwa Sasa Kuna njia nyingi za kujitangaza hasa katika mitandao ya kijamii kuwa na mahusiano mazuri na washirika katika biashara wengine ili kutambua mbinu mbalimbali za kibiashara.

Alisema kuwa mjasiriamali unatakiwa kuwa na ushirikiano na mwenzako na kuondokana na uadui ambao huweza kujenga chuki miongoni mwa wafanyabiashara kwani kukaa kwa pamoja na kujadili kunajenga hali ambayo kwenye biashara inakuza zaidi upeo kwenye biashara unayofanya.

 Aidha alitoa wito kwa wafanyabiashara wadogo kuwa na tabia ya kuweka kumbukumbu katika biashara unayofanya kuliko kutokuwa na kumbukumbu na mapato unayoiingiza na kuepukana na matumizi yasiyo na manufaa.

Kihongosi alisema mjasiliamali anatakiwa kuwa na mahusiana mazuri na mteja anayemhudumia kwenye matumizi sahihi ya lugha, huduma zilizo bora kwa lengo la kumteka zaidi anayemhudumia katika biashara anayofanya.

Aliwataka wajasiriamali kujenga uaminifu na sekta mbalimbali za kifedha ili waweze kusaidiwa kupata mikopo itakayowawezesha kusonga mbele zaidi na kupanua biashara wanazofanya..

Pia aliziomba taasisi mbalimbali za fedha kukopesha wajasiriamali ili waweze kujikwamua na hali za uchumi na kuwapunguzia riba ambazo zimekuwa chungu kwa wajasiriamali walio wengi.

Kihongosi aliwataka wajasiriamali kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha aua kuuza ndani na nje ya nchi kama fursa ya kupanua soko la bidhaa zao na kukua zaidi kutoka katika ujasiriamali mdogo kuwa mkubwa kuliko kubaki katika eneo moja bila malengo.

 

No comments :

Post a Comment