Saturday, November 7, 2020

MKUTANO WA BUNGE LA 12 KUANZA RASMI NOVEMBA 10,2020 JIJINI DODOMA

 

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuanza rasmi kwa Mkutano wa kwanza wa Bunge ambao utaanza Novemba 10,2020 jijini Dodoma.

PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG

…………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

KATIBU  wa Bunge Steven Kagaigai  ametangaza kuwa Bunge la 12 kuanza rasmi Novemba 10 mwaka huu jijini Dodoma huku akiwataka wabunge wa kuchaguliwa na kuteuliwa kufika katika

ofisi za Bunge wakiwa na nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kujisajili.

Wito huo ameutoa leo jijini Dodoma kwa waandishi wa habari jijini Dodoma Kagaigai  amesema kuwa  kikao hicho kimeitishwa baada ya Tangazo la Rais lililotolewa Novemba 5, mwaka huu kwenye gazeti la serikali toleo maalum namba 942A.

“Usajili wa wabunge unaanza leo Novemba 7 hadi 9 mwaka huu katika ofisi za Bunge jijini Dodoma ambapo amewataka wabunge kufika na nyaraka mbalimbali na kikao cha kwanza cha mkutano wa  bunge la 12 kitafanyika Novemba 10, mwaka huu kama ilivyotamkwa kwenye Tangazo la Rais,”amesema Kagaigai

Aidha Kagaigai amezitaja nyaraka hizo kuwa ni pamoja na Hati ya kuchaguliwa au kuteuliwa,nakala ya kitambulisho cha NIDA ,Kadi ya benki ya Mbunge  na cheti  cha ndoa kinachotambuliwa na serikali .

“Nyaraka nyingine ni cheti cha kuzaliwa cha watoto wenye umri chini ya miaka 18 kwa wenye watoto, vyeti vya elimu au taaluma ya mbunge a,bavyo husaidia namna ya kuwapanga wabunge katika kamati za bunge, picha ndogo (Passport size) nane na Nakala ya wasifu wa mbunge,”amesema Kagaigai

Hata hivyo Kagaigai amesema  kuwa shughuli zitakazofanyika katika mkutano huo ni pamoja na kusomwa kwa tangazo la Rais la kuitisha bunge,uchaguzi wa spika,kiapo cha umainifu kwa wabunge wote,kuthibitisha jina la waziri mkuu ,uchaguzi wa Spika na ufunguzi rasmi wa Bunge jipya utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

No comments :

Post a Comment