Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania Mabula Misungwi Nyanda, akizungumza na Maafisa wa TAWA waliofika katika kikao kazi Cha kujadili Mambo mbalimbali ya Mamlaka hiyo leo Mjini Morogoro.
Baadhi ya Maafisa wa TAWA waliohudhuria katika kikao kazi Cha kujadili Mambo mbalimbali ya Mamlaka hiyo wakimsikiliza Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania Mabula Misungwi Nyanda leo Mjini Morogoro.
Picha ya pamoja
Kati ya Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori
Tanzania Mabula Misungwi Nyanda na Baadhi ya Maafisa wa TAWA.
***********************
Na FARIDA SAID, MOROGORO
Baada ya tatizo
la muda mrefu la wanyama aina ya Tembo kuvamia kwenye makzi na kufanya
uharibifu wa mazao kwenye mashamba kisha kuua na kujeruhi watu katika
maeneo mbalimbali nchini, Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania
(TAWA) imeandaa mikakati ya kudhibiti wanyama hao kwa kuwashirikisha
wananchi na kuwapa mbinu za kujilinda dhidi ya wanyama hao.
Hayo yameelezwa
na Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori
Tanzania Mabula Misungwi Nyanda, wakati wa kikao kazi cha maafisa wa
mamlaka hiyo kwa lengo la kujadili masuala ya Bajeti pamoja na kuweka
mikakati madhubuti ya kulinda maeneo yote ya hifadhi ili yasitumiwe na
magaidi.
Amesema matukio
mengi yanatokana na wananchi kushindwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa
wanyamapori hasa inapotokea wanyama hao wamevamia kwenye mashamba au
kwenye makazi.
“tumekuwa tukitoa
maelekezo kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo yamekuwa wakiathiriwa
na wanyama kuwa inapotokea wananchi wamemuona tembo wajiepushe
kumkimbilia, kupiga kelele, kasha watoe taarifa kwenye mamlaka
zinazohusika kabla tembo hao hawajaleta madhara” kamishna mabula
alisema.
Hata hivyo kaimu
kamishna mabula amewaagiza wakuu wote wa vituo vya tawa kote nchini
kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya rushwa kwa baadhi ya askari kabla
hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao
“Hatutamvumilia
mkuu yeyote wa kito ambaye atakuwa anaona vitendo vya rushwa kwa baadhi
ya askari wa tawa na hachukui hatua badala yake tutaanza kwa
kumshughulikia yeye halafu askari wengine watauata” kamishna mabula
alisisitiza.
“lakini pia
katika mikakati ya tawa, tmejipanga kuhakikisha tunalinda mapori yetu
yote ili kuepuka matukio ya ugaidi kufanyika kasha magaidi kukimbilia
kwenye maeneo hayo na kuyafanya kuwa maficho na kuyageuza kuwa viwanja
vya mafunzo” kamishna mabula aliongeza.
Kwa upande wao
baadhi ya Maafisa wa TAWA waliohudhuria kakao hicho wamesema madhara
ambayo amekuwa yakijitokeza kwa wananchi kuvamiwa na kuuawa na wanaya ni
kutokana na uelewa ndogo wa wananchi hivyo wao kama watendaji
watahakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi hao.
Aidha katika
swala la rushwa Maafisa hao wamemuhakikishia kamishna Mabula kuwa
watakuwa waadilifu kila siku wawapo kazini kwani kutoa au kupokea rushwa
ni kosa kisheria,hivyo hawatojihusisha nayo.
No comments :
Post a Comment