Mkurugenzi Mkuu wa REPOA Dr.Donald Mmari akionyesha moja ya machapisho yaliyotolewa na tasisi ndani ya miaka 25
Mkufunzi wa Masuala ya Uchumi kutoka REPOA ,Dr.Blandina Kilama akitoa somo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari waliohudhuria mafunzo hayo ya siku Mbili
Mkurugenzi Mkuu wa REPOA (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Wahariri na Waandishi Waandamizi
HABARINa Al-Hassan Muhidin,Michuzi Tv
IMEELEZWA kwamba tafiti ambazo zimefanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini (Repoa) katika kipindi cha miaka 25 zimesaidia katika ufanikishaji wa kazi za Serikali kwa kipindi chote hichi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguaji wa semina ya siku mbili kwa Wahariri na waandishi wa habari iliyoandaliwa na taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dk. Donald Mmari amesema moja ya mafanikio waliyoyapata ni kuendelea kuwajengea uwezo watafiti.
Amesema wapo watafiti wengi waliopita kwao ambao kwa sasa ni walimu wa vyuo vikuu huku wengine wakifanya kazi katika mashirika ya kimataifa na Serikalini.
"Kiukweli mchango wa watafiti hawa tuliowajengea uwezo umeonekana na tafiti zao zimesaidia sana katika kufatilia jitihada za Serikali za kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa nchi," amesema Dk.Mmari.
Akizungumzia taasisi hiyo kutimiza miaka 25 amesema pamoja na Serikali,, sekta binafsi pia inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye tafiti kwa kuwa ndizo zinazotoa taswira ya uchumi.
Dk Mmari ameeleza katika kipindi cha miaka 25 ambacho Repoa imekuwa ikifanya tafiti, imechangia kwa kiasi kikubwa katika upangaji sera na mikakati ya maendeleo.
“Mchango wetu umechagia sana katika upangaji wa sera na mikakati ya maendeleo. Machapisho yetu yamekuwa yakijadiliwa kwa kina na tumeona mabadiliko ya kisera na kimkakati. Hapo ndipo tunaposema kwamba tafiti zina muhimu sio tu kwa serikali hata kwa wananchi. Mapendekezo yetu yamekuwa yakifanyiwa kazi,” amesema Dk.Mmari.
Ameongeza katika kipindi cha miaka mitano ijayo taasisi hiyo ina mpango mkakati uliojikita katika kuongeza juhudi za kujenga uweoz wa kufanya tafiti.
“Vyuo vinafanya tafiti ila inahitaji uzoefu na maarifa katika kufanya tafiti za kisera. Tumejikita katika kuongeza uwezo eneo hilo.Kuongeza kasi ya mafunzo kwa watumiaji wa tafiti wakiwemo watunga sera,” amesema Dk Mmari.
Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji huyo amesema katika miaka mitano hiyo Repoa itajikita zaidi kwenye kufanya tafiti za kimkakati na kuwajengea uwezo wa watafiti ili waweze kufanya kwa ufanisi tafiti za kisera.
“Tangu tumeanza kufanya kazi mwaka 1995 tumefanikiwa kutekeleza lengo letu la kushughulika na watafiti wa ndani hasa katika eneo la uchambuzi wa sera zinazohusu umaskini, tunaahidi kuongeza jitihada katika eneo hilo na tunajivunia kuona watu waliopitia hapa wanafanya shughuli zao kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo za kimataifa."

No comments :
Post a Comment