Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema ina mipango mikubwa na tayari imeshazungumza na benki ya dunia kwa ajili ya miradi mengine ili kuipendezesha Zanzibar na kuikuza kimaendeleo.
Hayo ameyasema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwenye uzinduzi wa jengo la MICHENZANI MALL huko Michenzani mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Bi. Sabra Issa Machano akitoa maelezo mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Michenzani Mall. Muonekano wa lift ndani ya jengo la Michenzani Mall Jiwe la Msingi wa jengo hiloAkitoa maelezo ya ujenzi wa jingo hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na mipango Ndg. Khamis Mussa Omar amesema “Mnamo mwaka 2013 mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ulianza ujenzi wa mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya mapinduzi katika eneo la Michenzani wakati wakiendelea na ujenzi huo mfuko uliona ipo haja ya kupeleka ombi Serikalini kwaajili ya kupatiwa eneo la biashara la makontenani ili kutanua uwekezaji wake wa ujenzi wa jingo la bishara ambalo litaendana na hadhi ya mnara ambapo ombi hilo lilikubaliwa na kupelekea kukabidhiwa rasmi eneo hilo la makontena kwa mfuko wa hifadhi ya jamii mnamo mwaka 2015” .
Baada ya kukabidhiwa eneo hilo hatua za uendelezaji zilianza rasmi. Ilipofika april 31, 2013 wafanyabiashara wa makontena waliondoka katika eneo hilo kupisha utekelezaji wa mradi wa Michenzani Mall”.
Itakumbukwa kuwa Octobar 4, 2018 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF ulitiliana saini na Kampuni ya CRJE East Afrika kwa ujenzi wa Jengo la Michenzani Shopping mall.
Jengo la Michenzani Mall limegawika katika maeneo makuu manne ambayo ni eneo la ghorofa ya chini ya ardhi, ghorofa ya pili, sehemu ya kati kati ya jengo , ghorofa ya tatu na sehemu mbili ya sehemu ya jengo zenye ghorofa tano kila moja
No comments :
Post a Comment