Monday, October 5, 2020

NBAA yatangaza matokeo ya mtihani ya 91 Mwezi Agosti 2020 ,

 

BODI ya Taifa ya Wahasibu  na Wakaguzi  wa Hesabu nchini NBAA,  imepitisha na kutangaza matokeo ya watahiniwa 5827  waliofanya mtihani

kati ya terehe 04 hadi terehe 07, Agosti ile iliyotakiwa kufanyika Mwezi Mei 2020 katika ngazi mbalimbali za masomo. Mtihani hii ilihairishwa kutokana na janga la Ugonjwa wa Homa kali ya mapafu(Corona) ulioenea ulimwenguni kote.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius  Maneno imebainisha kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 13 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Alisema mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya Pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa  Hesabu (ATEC I , ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya Awali/Msingi (Foundation Level) yenye masomo matano, Hatua ya Kati (intermiediate Level), yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne.

"Watahiniwa  waliosajiliwa  walikuwa  6,934 kati ya hao watahiniwa   1,107 sawa na asilimia  16.0 hawakuweza  kufanya  mitihani  hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo  watahiniwa   waliofanya   mitihani   walikuwa   5,827  sawa  na  asilimia

84.0.  Kati ya watahiniwa   waliofanya  mitihani  hiyo  watahiniwa   151 ambao ni asilimia 2.6 wamefaulu  mitihani  katika mkao mmoja, wengine  137  sawa na asilimia  2.4 wamefaulu  kwa  kufaulu  masomo  walioyokuwa   wameshindwa katika  mitihani  ya nyuma,  wengine  924  sawa  na  asilimia  15.9  wamefaulu mitihani  yao kwa  kufaulu  masomo  waliyokuwa   wamebakiza," alisema Maneno.   

Pia alisema  watahiniwa     1,214    sawa   na   asilimia    20.8   wamefaulu    mitihani    yao na kwamba watahiniwa   wengine   2,492  sawa  na  asilimia   42.8  wamefaulu   baadhi  ya masomo  katika  ngazi  mbalimbali  na watahiniwa  2,123  waliobakia   sawa na asilimia  36.4 hawakufaulu  mitibani  yao.

Awali, taarifa hiyo ilieleza kuwa watahiniwa waliosajiliwa    walikuwa   84  kati  ya  hao watahiniwa   10  sawa na asilimia  11.9  hawakuweza   kufanya  mitihani hiyo kwa  sababu  mbalimbali na hivyo kufanya ndani ya watahiniwa   waliofanya  mitihani kuwa  74   sawa  na  asilimia   88.1.     

Pia imeelezwa kuwa kati   ya  watahiniwa  74 waliofanya  mitihani katika ngazi hii watahiniwa 10  ambao ni asilimia 13.5  wamefaulu   mitihani  katika  mkao  mmoja huku wengine  08  sawa  na asilimia   10.8 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza,  wengine   18  sawa  na  asilimia  24.3  wamefaulu  huku watahiniwa 28 sawa na asilimia 37.8 wamefaulu baadhi ya masomo katika kazi hii na watahiniwa 28 waliobaki sawa na asilimia 37.8 hawakufaulu mitihani yao..   

Aidha, katika hatua ya  Kati, waliojisaliwa walikuwa   3,721   kati  ya  hao watahiniwa  618 sawa na asilimia 16.6  hawakuweza   kufanya  mitihani kutokana na sababu  mbalimbali. Hivyo watahiniwa  waliofanya  mitihani walikuwa 3,103 sawa na asilimia 83.4 Kati ya watahiniwa  3,103 waliofanya  mitihani  katika ngazi hii  watahiniwa   31 ambao ni asilimia 1.0  wamefaulu   mitihani   katika  mkao  mmoja,   wengine  99  sawa  na asilimia     3.2     wamefaulu     kwa     kufaulu     masomo waliyokuwa wameshindwa    katika   mitihani  ya  nyuma.

Alisisitiza wengine 528 sawa na asilimia 17.0 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza. Kwa ujumla watahiniwa 658 sawa na asilimia 21.2 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa   1,457  sawa  na asilimia    47.0   wamefaulu baadhi  ya masomo    katika    ngazi   hii. Watahiniwa    988  waliobakia   sawa  na  asilimia   31.8  hawakufaulu mitihani  yao.

Katika hatua ya mwisho, watahiniwa  waliosajiliwa walikuwa 2,245 kati ya hao watahiniwa 340 sawa na asilimia 15.1 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa  sababu mbalimbali. Hivyo hiyvo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 1,905 sawa asilimia 84.9.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo ametoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.

No comments :

Post a Comment