Monday, October 5, 2020

UFUNGUZI WA JENGO LA "ZSSF MICHENZANI MALL" ZANZIBAR WAFANA

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (wa pili kushoto) ambaye ni mgeni rasmi akijumuika na Viongozi mbali mbali katika kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la ZSSF Michenzani Mall ZANZIBAR Jengo linalomikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali
Hassan Mwinyi akisalimiana na Viongozi alipowasili katika hafla ya
Ufunguzi wa Jengo la ZSSF Michenzani Mall Mjini Zanzibar hafla
iliyofanyika leo.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) akisalimiana na Mgombea Urais wa
Zanzibar kupitia CCM Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika
Ufunguzi wa Jengo la ZSSF Michenzani Mall Mjini Zanzibar, jengo
lililojengwa na Kampuni ya CREJ kutoka Nchini China hafla
iliyofanyika leo viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani.

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilali mara alipowasili katika Ufunguzi wa Jengo la ZSSF Michenzani Mall  Zanzibar. 



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) pamoja na Viongozi wengine
wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa ZSSF
Sabra Issa Machano, wakati walipotembelea sehemu mbali mbali za Jengo la
ZSSF Mall Michenzani Mjini Zanzibar mara baada ya kulifungua
rasmi,hafla iliyofanyika leo Michenzani Mjini Zanzibar
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Mfuko wa ZSSF Nd, Sabra Issa Machano pamoja na Viongozi wengine wakati
alipotembelea sehemu mbalimbali za Jengo la ZSSF Michenzani Mall
Mjini Zanzibar mara baada ya kulifungua rasmi, hafla iliyofanyika leo
Michenzani Mjini Zanzibar.(Picha zote na Ikulu.)

 

No comments :

Post a Comment