Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano
la kimataifa la wanawake wajasiriamali lililofanyika mjini hapa.
Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza na wanawake wajasiriamali wakati
alipotembelea banda la mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wakionyesha
bidhaa zao jijini Arusha
Wanawake
wajasiriamali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya mkutano wa wajasiriamali wanawake uliofanyika mjini hapa.(Happy
Lazaro).
………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Anna Mghwira amewataka wanawake kupambania fursa za
uwekezaji katika biashara zao kwani wamekuwa na mchango mkubwa Sana
katika kuinua uchumi wa nchi.
Ameyasema hayo Jana
wakati akifungua kongamano kubwa la kimataifa la wanawake wajasiriamali
kutoka nchi mbalimbali barani ulaya na Afrika mashariki.
Mghwira alisema
kuwa,wanawake ni jeshi kubwa na wamekuwa wakidhubutu katika kushiriki
fursa mbalimbali za maendeleo Jambo ambalo kongamano hilo litawafanya
waendelee kujiinua kiuchumi na kuboresha biashara zao.
Amesema kuwa,wanawake
wanapaswa kujiongeza katika shughuli zao na kuhakikisha kuwa
wanaongezea thamani bidhaa zao ili ziweze kupata soko ndani na nje ya
nchi na kuweza kupanua wigo wa biashara zao.
“wanawake wanapaswa
kuendelea kupambana katika kujimarisha katika Masoko ya nje kwa lengo la
kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani wa nje kwani kazi nyingi
zinazo zalishwa nchini zina ubora wa kiwango cha kuuza nje,hivyo ni
wajibu wao kuhakikisha kuwa wanakuwa na udhubutu wa kutosha na kuboresha
bidhaa zao ili zijulikane kimataifa.
Kwa upande wake
Gladness Katega ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Iamwomenprenear
LTD,ambaye pia ni Mratibu wa kongamano hilo amesema kwamba lengo la
kuwakutanisha Wanawake hao ni kujijengea uwezo pamoja na kutambua fursa
za kufanya biashara ndani na nje ya nchi kwa kuwakutanisha wanawake
mbalimbali kutoka nchi za nje ambao wamefanikiwa kibiashara.
Katega amesema kuwa,
kongamano hilo limelenga kuwafundisha wanawake namna ya kupambana na
Biashara kimataifa na kitaifa na kufikia malengo ya kukuza biashara zao
kwa mtandao lengo likiwa ni kuhakikisha bidhaa zao zinafikia wateja
nje ya Mkoa wa Arusha na sehemu zingine nchini.
Aliongeza
kuwa,wanataka kuhakikisha mafunzo watakayopata kwenye kongamano hilo
yatawawezesha namna ya kukuza biashara zao na kuweza kupata soko la
uhakika ndani na nje ya nchi na kuweza kujulikana kitaifa.
Baadhi wa washiriki
wakiongelea Kongamano hilo na namna watakavyo nufaika Rejea Vivao
walisema kuwa,kitendo Cha kuwakutanisha wanawake hao kimeleta manufaa
makubwa Sana kwani wameweza kubadilishana uzoefu na wenzao wa nje ya
nchi namna ya kuboresha biashara zao na kuzifanya ziwe za kimataifa
zaidi.
Aliongeza kuwa
,kikubwa zaidi ni kuwa wanategemea kupata mafunzo yatakayo wasaidia
kusonga mbele katika biashara zao na kufikia masoko makubwa ya nje hasa
kwa kutumia mitandao.
No comments :
Post a Comment