………………………………………………………………..
Kiasi cha shilingi
bilioni 28 kitatumika kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa stendi ya kisasa
ya mabasi na malori inayojengwa katika kata ya Nyamhongolo wilaya ya
Ilemela ili kukuza uchumi na kupunguza changamoto ya ajira.
Hayo yamebainishwa na
Naibu waziri wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ambae
pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia chama cha mapinduzi
Dkt Angeline Mabula wakati alipotembelea stendi hiyo kufuatilia
utekelezaji wa mradi huo kabla ya kuzungumza na wananchi wa kata ya
Nyamhongolo katika muendelezo wa mikutano yake ya kampeni kueleza juu ya
miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya CCM kwa
kipindi cha miaka mitano ambapo amesema kuwa mradi huo wa stendi ya
kisasa umeweza kuajiri zaidi ya watu 206 wenye utaalamu na wasio na
ujuzi rasmi huku akiwaomba wananchi wa kata hiyo kutumia fursa ya uwepo
wa mradi huo kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara na kuanzisha
miradi mingine ndani na jirani ya stendi hiyo
‘ Tujiandae tukawekeze pale kwenye mradi ule wa stendi utakapokamilika, tusiogope tuombe vyumba vya biashara ‘ Alisema
Aidha Dkt Mabula
akaongeza kuwa amefurahishwa na uwepo wa mkakati wa ujenzi wa eneo la
kufanyia biashara wajasiriamali wadogo wadogo maarufu kama machinga
jirani na stendi hiyo jambo litakalosaidia kupunguza migogoro isiyokuwa
ya lazima kama inayojitokeza maeneo mengi ya mijini kutokana na
kukosekana kwa maeneo rasmi ya wafanya biashara hao.
Kwa upande wake
msimamizi wa mradi huo Mhandisi wa manispaa ya Ilemela Ndugu Juma
King’ora akafafanua kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema mwezi
Mei na mpaka sasa umeshafikia asilimia 52 ya utekelezaji wake.
Huku msanifu majengo
ambae pia ni msimamizi msaidizi wa mradi huo Ndugu Hellen Mgalula
akisema kuwa mradi huo ulitarajiwa kukamilika mapema zaidi kabla ya muda
uliopangwa sasa lakini changamoto za kuzuka kwa ugonjwa wa homa ya
mafua makali inayojulikana kama Covid-19 na uwepo wa maji mengi eneo la
mradi umechangia kuongeza siku za kukamilika kwake.
No comments :
Post a Comment