Mwezeshaji/Mwanasheria Neema Ahmed akizungumza wakati wa
mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wasaidizi wa kisheria
ambapo aliwasititiza kuepuka kufanya usuluhishi wala upatanishi kwenye
kesi zinazohusu makosa ya jinai.
Mwezeshaji/Mwanasheria Neema Ahmed akizungumza wakati wa
mafunzo ya siku tatu yaliyoanza leo kwa Wasaidizi wa Kisheria 27 kutoka
Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na TGNP kwa
kushirikiana na UNFPA na KOICA yakiratibiwa na shirika la PACESHI yakiwa
na lengo la kukuza uelewa wao kwenye masuala ya kijinsia na namna gani
watashiriki katika harakati za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na
watoto kwenye jamii.
Mwanasheria Jenisia Mavere ambaye ni miongoni mwa
wawezeshaji akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza leo
kwa Wasaidizi wa Kisheria 27 kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na
Kishapu yaliyoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na UNFPA na KOICA
yakiratibiwa na shirika la PACESHI yakiwa na lengo la kukuza uelewa wao
kwenye masuala ya kijinsia na namna gani watashiriki katika harakati za
kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye jamii.
Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada
wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija
kutoka Shirika la PACESHI la Shinyanga mjini akizungumza wakati wa
mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Ushetu na
Kishapu yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na
KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya
kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada
wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija
kutoka Shirika la PACESHI la Shinyanga mjini akizungumza wakati wa
mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Ushetu na
Kishapu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.
Msajili Msaidizi wa Watoa Huduma
ya Msaada wa Kisheria halmashauri ya wilaya ya Kishapu Efrem Kilango
akizungumza katika mafunzo hayo ambapo alisema majukumu ya Wasaidizi wa
kisheria pamoja na kusaidia jamii za maeneo yao kuhusu masuala ya
kisheria hususani ukatili wa kijinsia na pale Msaidizi wa Kisheria
anapoona shauri limeshindikana atoea rufaa kwenda ngazi za juu kama
ofisi za maafisa watendaji wa kata,vijiji, polisi au mahakamani.
Msajili Msaidizi wa Watoa Huduma
ya Msaada wa Kisheria halmashauri ya wilaya ya Kishapu Efrem Kilango
akizungumza katika mafunzo hayo.
Wasaidizi wa Kisheria kutoka
Halmashauri ya Ushetu na Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na
wawezeshaji wa mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia
Wasaidizi wa Kisheria kutoka
Halmashauri ya Ushetu na Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na
wawezeshaji wa mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wakili Neema Ahmed
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wasaidizi wa Kisheria
‘Paralegals’ wametakiwa kuepuka kufanya usuluhishi wala upatanishi
panatokea matendo ya ukatili wa kijinsia ambayo ni makosa ya jinai
badala yake wapeleke mashauri ya jinai kwenye ngazi zinazostahiki
ikiwemo Dawati la jinsia na watoto,polisi au kwa walinzi wa amani wa
maeneo husika.
Rai hiyo imetolewa leo Jumapili
Oktoba 4,2020 Mjini Shinyanga na Wakili Neema Ahmed wakati wa mafunzo ya
siku tatu yaliyoanza leo kwa Wasaidizi wa Kisheria 27 kutoka
Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na TGNP kwa
kushirikiana na UNFPA na KOICA yakiwa na lengo la kukuza uelewa wao
kwenye masuala ya kijinsia na namna gani watashiriki katika harakati za
kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye jamii.
“Msaidizi wa Kisheria
ukiletewa Mashauri ya jinai kama vile ya
vipigo,ubakaji,ulawiti,mashambulio ya aibu,tafadhali usifanye usuluhishi
wala upatanishi bali yapeleke kwenye ngazi za ili hatua zichukuliwe
dhidi ya wahusika wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake”,alisema Neema.
“Makosa ya jinai
hayasuluhishwi. Msaidizi wa Kisheria unasuluhisha jinai kama nani?, mtu
anasema amepigwa unaanza kufanya usuluhishi ili iweje? Kama ni kosa la
jinai unatakiwa kwenda polisi au kwa afisa mtendaji wa kata au kijiji
ili wao wawasiliane na polisi kwa ajili ya hatua zaidi. Jukumu lako ni
kuwaeleza waende kwenye maeneo husika”,aliongeza Neema.
Mwanasheria huyo aliwaasa
wasaidizi wa kisheria pale wanapopokea kesi za jinai wasikubali
kusuluhisha,wawambie wahusika waende kwenye dawati la jinsia au kwa
walinzi wa amani wakiwemo maafisa watendaji kata na vijiji huku
akiwasisitiza kuwa hata upelelezi wa kesi za jinai siyo sehemu ya
majukumu yao.
Nao Wasaidizi wa kisheria
walioshiriki katika mafunzo hayo wameyataja mashauri/kesi zinazoongoza
kuwafikia ni zile zinazohusu masuala ya ardhi,mirathi, migogoro ya ndoa
na matunzo ya watoto.
Hata hivyo walizitaja baadhi ya
changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na wahanga wa matukio ya
ukatili wa kijinsia kuogopa kutoa ushirikiano,waathirika kuwa wasiri
hawataki kuongea yanayowasibu lakini pia baadhi ya Wasaidizi wa kisheria
wanapata vitisho wanapofuatilia baadhi ya kesi.
No comments :
Post a Comment