Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna akizungumza. Kuhusiana namna
wqlivyojipanga katika mpango wa Dunduliza kwa wananchi kuchangia kidogo
kidogo ili kuweza kujiunga na huduma za matibabu ya NHIF.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF Bernard Konga akishikana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya NMB Ruth Zaipuna Mara baada kusaini makubaliano katika uzinduzi
wa mpango wa Dunduliza uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF Bernard Konga (katikati) wakionesha mabakubaliano na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna katika uzinduzi uliofanyika
jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja kati ya NHIF na Benki ya NMB Mara baada ya kusaini makubaliano.
*Wananchi kujiunga na huduma za matibabu za NHIF
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Benki ya NMB
wamezindua mpango unaojulikana Dunduliza unaowezesha wananchi
kudunduliza fedha kidogo kidogo za mchango wa bima ya afya na hatimaye
kufanikisha kuchangia kiwango kinachotakiwa na kujiunga na huduma za
bima ya afya kupitia NHIF.
Uzinduzi
huo umefanyika Dar es Salaam ambapo pia uzinduzi umeambatana na kusaini
makubaliano (MOU) kati ya NHIF na Benki ya NMB ya namna ya wateja
watakavyoweza kuchangia ama kujiwekea fedha kwa ajili ya kukamilisha
mchango wa huduma anazohitaji.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Bernard Konga amesema mpango wa Dunduliza unawezesha wananchi wa
wanaojiunga na NHIF kupitia mpango wa vifurishi kuweka fedha kidogo
kidogo kupitia Benki ya NMB kwa muda atachagua na atakakamilisha kiwango
husika atapatiwa kadi ya matibabu na kuanza kunufaika na huduma za
matibabu kupitia NHIF.
Amesema
mwananchi anayehitaji kujiunga na huduma za NHIF ambaye anahitaji
kuweka fedha kidogo kidogo kupitia banki ya NMB kwa muda atakaochagua na
atakakamilisha kiwango husika atapatiwa kadi ya matibabu na kuanza
kunufaika na huduma za matibabu kupitia NHIF.
Amesema
mwananchi anahitaji kujiunga na huduma za mfuko wa Taifa wa Bima ya
afya ambaye atahitaji kuweka fedha kidogo kidogo kwa muda atakaochagua
ni yule anajiunga kupitia mpango wa vifurishi ambavyiuvinajulikana kwa
majina ya Najali Afya, Wekeza afya na Timiza afya ambavyo pia vina mpa
fursa mwananchi anayehitaji kuchangia kuchagua huduma kulingana na
mahitaji yake, umri na wanufaika wanaohitaji kuwajumuisha.
Amesema
mpango huu unawezesha mwananchi kujiwekea fedha kwa ajili yake Mwenyewe
ama kwa ajili yake na mwenza wake na mtoto ama Watoto alionao.
Amesema mfumo huo haubagui mwananchi yoyote kulingana na aina ya simu aliyonayo na endapo atakwama katika hatua za kujisajili.
Amesema
wakati mfuko unazindua mpango wa vifurushiu Novemva mwaka jana,
changamoto iliyionekana ni pamoja na uwezo wa wananchi kulipa fedha zote
kwa awamu moja hatua iliyoifuata Menejimenti ya mfukonkufungua milango
na kuanza kushirikiana na wadau wa Taasisi za kifedha kama NMB ambayo
ina wigo mpana kwa nchi.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ruth Zaipuna amesema anafarijika kuzinduliwa
kwa mpango huo ambao anaamini utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kuwa
ndani ya mpango wa NHIF lakini pia kuwajengea wananchi tabia ya
kujiwekea akiba kwa matumizi yanye manufaa ya baadaye kwao.
"Afya
ni kila kitu na hata kwa upande wetu sisi Benki, tunahitaji Sana wateja
ambao Wana uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote na sio wa
kuchujua akiba zao Benki kwenda kujitibia, niombe Sana wananchi
tuutumie huu mpango kuhakikisha wengi wetu tunajiwekea fedha na hatimaye
kupata kadi ya matibabu."Amesema Bi Zaipuna
No comments :
Post a Comment