Friday, September 4, 2020

WORLD VISION YAWANOA WANAHABARI KUHUSU LISHE NA AFYA YA UZAZI


Meneja
wa Mradi wa ENRICH, Bi Mwivano Malimbwi (aliyesimama) akitoa mafunzo
maalum ya malengo ya mradi huo ya utoaji wa elimu ya lishe na kuboresha
afya ya uzazi kwa vijana balehe kwenye  mikoa ya Singida na Shinyanga
kwa waandishi wa habari ya Mkoa wa Singida (hawapo pichani)
leo, aliyekaa  ni mtaalam wa Jinsia na Utetezi wa Mradi Huo Tumaini
Fred
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia mazao ya asali na
mashine ya kukamulia asali  ya kikundi cha ufugaji wa nyuki mkoani
Singida kinachofadhiliwa wa World Vision hivi karibuni
Na. John
Mapepele
,Singida
Shirika la
World Vision nchini  limewataka waandishi wa habari kama wadau wakuu wa
Shirika  hilo
kutoa taarifa sahihi za kazi za
shirika hilo  kwenye mradi wake wa
ENRICH  ambao unatekelezwa  katika
mikoa ya Singida na Shinyanga.
Mradi huo unalengo la kupeleka elimu ya lishe na
afya ya uzazi kwa vijana balehe vijijini ili kupunguza  vifo vya akinamama wajawazito na watoto
chini  ya siku 1000 na  ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya
Awamu ya Tano ili kuboresha maisha ya watanzania.
Akitoa mafunzo
maalum  kuhusu malengo wa mradi kwa
waandishi wa Mkoa wa Singida , Meneja wa Mradi wa ENRICH  Bi, Mwivano Malimbwi amesema mradi huu  ni  wa
miaka mitano  kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka  2021 na umejikita katika  kuwezesha
huduma za lishe ili kuimarisha afya
ya  mama na mtoto  kwa gharama za dola  milioni 8.4 za kikanada.
 Kwa mujibu wa Malimbwi  malengo
mahususi ya ENRICH ni kupunguza  vifo vya akina mama na watoto  kwa kuangalia
visababishi  vya vifo hivyo ambapo
mradi umeelekeza nguvu kwenye kuimarisha mifumo ya utoaji wa afya katika vituo
vya kutolea  huduma  hizo.
Aliongeza kuwa
awali wakati mradi ulipoanza
walibaini  changamoto ya
upatikanaji wa vifaa vya kumchunguza hali ya kiliishe ya mtoto  vilikuwa na upungufu mkubwa ambapo  vituo vichache  vilikuwa na
vifaa hivyo vya kupimia urefu na mzingo wa kati wa mkono kwa akina mama
na mtoto
Alisema kuwa watoa huduma wachache walipata mafunzo ya afya ya lishe  kwenye ngazi ya mkoa na wilaya ambapo  hakukuwa na watoa huduma katika maeneo ya
vijijini.
Aidha alisema pia hakukuwa na elimu ya uongozi kwenye kamati za afya za mikoa  na wilaya ambapo Mradi uliwajengea uwezo ili
kuwa sehemu ya  kuleta mabadiliko kwa
pamoja  badala ya kuwa watoa maamuzi. 
Aidha mipango na bajeti ilikuwa ikifanywa kwa hisia  badala ya kutumia takwimu sahihi.
Malimbi amesema
lengo la  pili  la Mradi ni kuongeza uzalishaji wa
chakula  chenye uwingi wa virutubisho
ambapa kwenye eneo hili amessisitiza kuwa mkakati umekuwa  katika kuongeza  uzalishaji ulioongezwa kibailojia, kuongeza
utumiaji wa virutubishi kwa watoto na sayansi ya ulaji na ufyonzaji wa
virutubishi,
Alisema pia katika mikoa ya Singida na Shinyanga imebarikiwa kuwa na  vyakula vya makundi yote na matunda ya asili
kama sasati, rade na furu ambayo kama yakitumika kikamilifu yatasaidia sana
kuboresha lishe na kupunguza udumavu kwa watoto.
Alipongeza
jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Dk. Rehema Nchimbi  kuwa  mstari
wa mbele katika kuhakikisha kuwa suala la lishe na afya ya uzazi vinakuwa
kipaombele cha kwanza kwa wananchi ambapo pia amesema amehamasisha ulaji na
ulimaji wa viazi lishe na kuwafanya wananchi wa Mkoa wa Singida tofauti na
awali ambapo vilikuwa vikiuzwa nje ya Mkoa.
Aidha amesema
Mradi umehamasisha akina mama kulima bustani za mbogamboga kwenye kila kaya ili
kuhakikisha kuwa  kwenye kila mlo mboga
zinakuwepo.
Amesema lengo
la mwisho la mradi  huo  ni kuhakikisha  kuwa
kunakuwa na uwajibikaji wa wadau wote muhimu na kila mmoja anafanya
majukumu yake kwa ufasaha, ambapo ametolea mfano kuwa Serikali kama mdau mkuu
ina wajibu wa kuweka  vituo vya kutolea
huduma na mtoa huduma ambapo jamii inawajibu wa kuvitumia vituo hivyo na
watoa  huduma.
Mradi wa ENRICH
ni Mradi wenye sekta nyingi na unafadhiliwa na Serikali ya  nchi ya Canada ambapo unatekelezwa kwa
kushirikiana  na wabia ambao ni
Nutritional International, Canadian Society for  International Health anayejikita katika
kuimarisha mfumo wa afya.
Ikiwemo Harvest Plus, kwenye Sekta ya Kilimo, Chuo kikuu cha
Toronto  katika kufanya tathimini na
ufuatiliaji wa mradi na World Vision ambaye ni msimamizi mkuu wa fedha wa mradi
huo. Serikali ya Tanzania ni mtekelezaji namba moja chini ya TAMISEMI.

No comments :

Post a Comment