Baadhi ya Wataalamu wa huduma za
ugonjwa wa sikoseli kutoka chuo cha afya (MUHAS) wakiwa katika hospitali
ya Wilaya ya Bgamoyo kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu katika
kiliniki maalumu ya ugonjwa huo ambayo itakuwa inapatikana kila siku ya
jumatatu.
Mratibu wa huduma ya Sikoseli
kutoka Chuo cha afya Muhimbili (MUHAS) Dk. Agnes Jonathan,akitoa elimu
kwa baadhi ya wagonjwa waliokwenda kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa wa
sikoseli sambamba na kuwaelekea namna ya wazazi kuwahudumia watoto wao
pindi wanapokuwa na ugonjwa huo.

Mratibu wa huduma ya Sikoseli
kutoka Chuo cha afya Muhimbili (MUHAS) Dk. Agnes Jonathan,akifafanua
jambo kwa wazazi, walezi pamoja na wananchi wengine ambao walifika
katika kiliniki maalumu ambayo imezinduliwa kwa ajili ya kutibu ugonjwa
wa sikoseli katika hospitali ya Bagamoyo.(PICHA ZOETE NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, BAGAM,OYO
Jopo la wataalam
wa Afya kutoka Chuo cha Afya Muhimbili (MUHAS) kupitia program ya ya
selimundu wakiongozwa na Dk. Agnes Jonathan, hatimaye wameanza rasmi
zoezi la utoaji wa
huduma katika kliniki maalum kwa wagonjwa wa
sikoseli katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani.
Lengo la
kuanzishwa kwa utaoji wa huduma hiyo imekuja ikiwan imepita miezi
miwili tu tangu Serikali kuzindua mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu
wenye ugonjwa wa sikoseli mnamo Juni 19,2020 kwa lengo la kuweza
kusaidia kutoa huduma kwa wagonjwa mbali mbali wanaosumbuliwa na
sikoseli katika Wilaya hiyo.
Katika
kukabiliana na ugonjwa huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu aliagiza kuanzishwa kwa kliniki
maalumu za kuchunguza ugonjwa huo katika ngazi ya wilaya na mikoa ili
kuhakikisha watu wengi hasa watoto wanafikiwa kwa urahisi kupatiwa
huduma hiyo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed
Farah alisema kwamba anashukuru sana kwa kuzinduliwa kwa mpango huo
ambao utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa ambao wamekuwa
wanasumbulia kwa kipindi kirefu na kusumbuliwa kwa sikoseli.
“Kwa kweli
napenda kutoa shukrani zangu za kipekee kwa kuanzishwa kwa utoaji wa
huduma hii katika hospitali yetu ya Bagamoyo kwani kutaweza kutoa fursa
ya kipekee kwa wananchi wa Bgamoyo kupitia wataalamu ambao wamefika
kupata huduma ya matibabu ya sikoseli ambapo wataondoka na changamoto
ya kwenda kutibiwa sehemu nyingine,”alisema Dk. Farah.
Pia alifafanua
kuwa kuzinduliwa kwa kliniki hiyo katika Hospitali ya Bagamoyo kupitia
mpango ambao umeanzishwa na serikali kutawapa urahi kwa wagonjwa mbali
mbali ambao wanasumbulia na sikoseli kupata matibabau yao kwa uharaka
zaidi kuliko na ilivyokuwa katika kipindi cha mwanzoni.
Naye mratibu wa
program ya sikoseli kutoka Chuo kikuu cha afya Muhinbili (MUHAS)
Dk.Agnes Jonathan alibainisha kwamba jamii hususan wazazi kuwapelekea
watoto wao mapema kupatiwa matibabu ya sikoseli endapo watabaini kuwa
anadalili za ugonjwa huo lengo ikiwa ni kumpatia matibabu ya haraka.
“Kumekuwepo kwa
baaadhi ya jamii kuwa na mwennendo wa tabia ya kuwa na dhana ptofu
kuhusiana na ugonjwa huu wa sikoseli lakini ni vizuri tukajiwekea
utaratibu wa kuwapeleka wagonjwa hospitalini ili waweze kupatiwa
matibabu ikiwemo sambamba na kwenda kupima afya zao mara kwa
mara,”alisema Dk. Agnes.
Bi. Arafa Said ni
Mwanzilishi na Rais wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojulikana kwa
jina la Sickle cell Disease Patiebts Community of Tanzania amewaomba
wazazi na kuwatia moyo wenye watoto ambao wanasumbuliwa na ugonjwa huo
waondoe hofu na mashaka kwani wakizingatia ushauri kutoka kwa wataalamu
wa afya wanawezeza kusihi maisha marefu bila tatizo.
Mwongozo wa Taifa
wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa Sikoseli ulizinduliwa rasmi Juni
19 mwaka huu na Waziri wa afya maendeleo jinsia wazee na watoto Mh.
Ummny Mwalimu katika hospitali ya Taifa ya muhimbili ukiwa na kauli mbiu
inayosema “Huduma bora kwa kila mhitaji, chukua hatua panua wigo.
No comments :
Post a Comment