
*************************************
Kampuni ya Tanzania Breweries
Public Limited Company(TBL Plc) imezindua kampeni ya kuhamasisha
utumiaji wa vinywaji vyenye kilevi kistaarabu inayojulikana kama ‘Pombe
sio Chai, Kunywa Kistaarabu’.
Kampeni hii imelenga kubadili
tabia za watumiaji wa bidhaa za pombe kutambua tofauti ya
unywaji wa
kupita kiasi na unywaji wa kistaarabu na itafanyika kwa kuelimisha faida
za unywaji wa kistaarabu kupitia njia mbalimbali zikiwemo
redio,magazeti,njia za mitandao ya kijamii ya kidigitali na kampeni za
moja kwa moja kwa wateja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL
Plc, Philip Redman alisema “Tukiwa kampuni inayoongoza kwa kutengeneza
vinywaji nchini, tunaamini ni jukumu letu pia kuhamasisha watumiaji wa
bidhaa zetu nchini Tanzania kubadilisha mienendo yao kwa kuzitumia
kistaarabu. Mkakati wetu wa kutoa elimu hii umelenga kubadili tabia za
watumiaji katika jamii na kufanikisha sera ya biashara yetu ya kuleta
mabadiliko chanya kwa kujenga jamii inayotumia vinywaji kistaarabu’’.
Aliongeza kusema kuwa kampeni ya ‘Pombe sio Chai, Kunywa
Kistaarabu’ itajikita kwenye masuala ya athari za matumizi ya pombe
kupita kiasi kwa watu wazima, matumizi ya pombe kwa wenye umri mdogo na
makundi maalumu kwenye jamii kama wajawazito, matumizi ya vinywaji
ambayo yanaweza kuleta madhara kwa watu wengine kama kuendesha vyombo
vya moto ukiwa umelewa.
“Tunaamini kuwa matumizi ya bia
yawe na matokeo chanya na ndio maana tunahimiza watumiaji na wateja kwa
ujumla kunywa kistaarabu’, aliongeza kusema Redman.
Kwa kipindi cha muda mrefu kampuni
ya TBL imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya unywaji wa kistaarabu
katika makundi mbalimbali ya jamii. Dira ya kampuni ni kuendesha kampeni
zenye kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii katika maeneo inakofanyia
biashara zake.
No comments :
Post a Comment