Mkoa
wa Kagera ni miongoni mwa mikoa inayolima na kuzalisha kwa wingi zao la
Kahawa hapa nchini ambapo imeelezwa kuwa pamoja na uzalishaji huo
wananchi wa mkoa huo hawana utamaduni wa kunywa kahawa wanayoilima wao.
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasema hayo jana Tarehe 4 Septemba 2020
alipofanya ziara katika kiwanda cha kahawa cha AMIMZA kilichopo
halmashauri ya wilaya Bukoba Mkoani humo ambapo amesema kuwa wananchi wa
mkoa huo ni wakulima wazuri wa kahawa ila sio watumiaji wa kahawa yao.
“Wananchi
wa Bukoba pamoja na watanzania kwa ujumla wake kama wangeweza kutumia
ipasavyo kahawa yao tusingekuwa na tatizo la masoko ya kahawa, hivyo
nawasihi wananchi wenzangu kuhakikisha kuwa mnatumia kahawa ipasavyo ili
kuimarisha soko letu la ndani” Amesema Waziri Hasunga
Hasunga
ameongeza kuwa Kahawa inayolimwa Kagera imekuwa Kahawa bora Duniani
ambayo hupelekea baadhi ya makampuni huko ulimwenguni kuitumia kwa
kuiwekea Lebo nyingine ambao hunufaika Zaidi na kahawa yetu kutokana na
faida zilizopo kwenye zao hilo.
“Watanzania
hasa wanakagera hawana utamaduni wa kunywa kahawa pamoja ya kuwa sisi
wenyewe ni wazalishaji wa kubwa wa Kahawa hapa nchini, naona ipo haja ya
watu wetu kuelimishwa faida za unywaji wa kahawa. Lakini nawapongeza
sana kwa uwekezaji mkubwa mlioufanya hapa Kagera.” Amesema Waziri
Hasunga
Ameongeza
kuwa mkoa wa Kagera unayo fursa nyingi za uwekezaji hasa za viwanda na
kuwasihi wawekezaji kujitokeza kwa kuwa usalama ni wa kutosha na
kuongeza kuwa zao la kahawa linatakiwa kuwa zao bora nchini kama
watanzania wataamua kulipa umuhimu na nafasi.
Kwa
niaba ya mmiliki wa kiwanda cha AMIMZA Ndg Billal Amir Hamza amesema
kuwa amesema kuwa kiwanda hicho kipo katika maboresho kwa kuongezea
baadhi ya idara na kuongeza kuwa kikikamilika kitaweza kutoa ajira kwa
watanzania Zaidi ya 600.
Billal
ameongeza kuwa kiwanda kikikamilika kitaweza kuzalisha kahawa mumunyifu
(Instant) tani 6,000 sawa na tani 18,000 za kahawa safi ambazo ni sawa
na tani 36,000 za kahawa ya maganda ambayo ni mara mbili kutokana na
gredi ya kahawa.
“Mpaka
sasa pamoja na uzalishaji unaoendelea tumeajiri wafanyakazi 59 pamoja
na kutoa ajira nyingine kwa wananchi ambao ni majirani zetu hapa ambapo
pia tumejenga kiwanda kikubwa Africa Mashariki na kati, niseme tu sisi
soko letu lipo nje ya nchi ila kwasasa tumerudi nyuma baada ya janga
hili la Covid-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona baada ya baadhi ya
nchi kufunga mipaka yake.” Amesema Billal
No comments :
Post a Comment