Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Matrekta na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu uliofanyika katika Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) eneo la Makutupora Jijini Dodoma leo tarehe 1 Septemba 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Matrekta na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu uliofanyika katika Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) eneo la Makutupora Jijini Dodoma leo tarehe 1 Septemba 2020.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Hunges Motors Tanzanaia Ndg Alex Duffar akitoa
maelezo ya kina kuhusu matrekta New Holanda mbele ya Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga mara baada ya kuzindua Matrekta saba na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu uliofanyika katika Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) eneo la Makutupora Jijini Dodoma leo tarehe 1 Septemba 2020.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akimsikiliza
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Hunges Motors Tanzanaia Ndg Alex
Duffar kuhusu matrekta New Holanda mara baada ya kuzindua Matrekta saba na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu uliofanyika katika Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) eneo la Makutupora Jijini Dodoma leo tarehe 1 Septemba 2020.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akikagua shamba la zabibu mara baada ya kutembelea Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kwa ajili ya uzinduzi wa Matrekta saba na zana zake uliofanyika katika eneo la Makutupora Jijini Dodoma leo tarehe 1 Septemba 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Katika
mwaka 2019/2020, Serikali kupitia Programu ya Uendelezaji wa
Sekta ya
Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) katika fedha zake za maendeleo pamoja na
mambo mengine ilitenga fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya
mashamba ya utafiti na uzalishaji wa mbegu bora kwa lengo la kuchangia
upatikanaji wa mbegu bora ili kukidhi mahitaji ya Wakala wa Mbegu (ASA),
Makampuni binafsi yanayohitaji mbegu za awali kutoka TARI, na hatimaye
kusambazwa kwa wakulima.
Mwaka 2019/2020, Serikali imetoa fedha
za kuweza kununua matrekta saba (7) na zana zake ambazo zitatumika
katika kupanua mashamba ya uzalishaji wa mbegu na miche bora ya mazao na
pia kuimarisha mashamba ya utafiti kwa kuzalisha aina mpya za mbegu
bora za mazao mbalimbali.
Wizara ya Kilimo,
kupitia ASDP II imeendelea kuimarisha mazao ya Kimkakati ikiwa ni
pamoja na Michikichi, Korosho, Pamba, Ngano, Mkonge, Alizeti, Mahindi,
Mtama, Uwele na Zabibu. Aidha, Mikakati hii ya Wizara chini ya ASDP II
imechagiwa zaidi na msisitizo wa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassimu
Majaliwa Majaliwa ambaye amehamasisha uzalishaji wa kilimo cha
Michikichi na Mkonge hapa nchini. Katika uhamasishaji huo, Wizara
kupitia TARI imeweza kuzalisha miche milioni 2 kwa mwaka 2019/2020 na
inategemea kufikia miche milioni 41 mwaka 2025.
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 1 Septemba 2020
katika eneo la Makutupora Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Matrekta
na zana zake ili kuimarisha uzalishaji wa mbegu unaofanywa na Taasisi ya
utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) na kuongeza kuwa hatua hizo zinazochukuliwa na Serikali zitakidhi mahitaji ya mbegu nchini.
Amesema kuwa Matreka hayo yaliyozinduliwa yamelengwa
kuongeza uwezo wa TARI katika kuzalisha mbegu bora kutoka takribani
tani 1,000 kwa sasa hadi kufikia tani 10,000 mwaka 2025. Vile vile,
katika kipindi hicho, TARI itaweza kuzalisha miche kutoka milioni 10.3
ya sasa hadi kufikia miche milioni 40 mwaka 2025.
Waziri
Hasunga amesema kuwa upatikanaji wa matrekta hayo utaimarisha
upatikanaji wa mbegu mbalimbali ikiwemo mbegu za Michikichi
zitakazoiwezesha serikali kuwa na utoshelevu wa mafuta ya kula.
Ameongeza kuwa ili kuwe na usalama wa chakula ni lazima msisitizo mkubwa uwekwe kwenye usimamizi madhubuti kwenye sekta ya mbegu ili kuwe na mbegu bora za kutosha na zenye bei nafuu kwa wananchi.
Waziri
Hasunga amesema kuwa Serikali imekusudia kuongeza uzalishaji wa mbegu
mbalimbali za nafaka, Mboga na matunda kadhalika mazao ya mafuta
Hasunga
amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia
kuhakiisha inaongeza juhudi za kuchakata mazao yatokanayo na kilimo ili
kuongeza thamani ya mazao na hatimaye kuimarisha upatikanaji wa
malighafi za viwandani.
No comments :
Post a Comment