Wauguzi wa hospitali ya Rufaa ya
Mkoa ya Mount Meru-Arusha wakionesha vyeti vyao mara baada ya
kutunukiwa vyeti kama ishara ya kuwatambua kwa kutoa huduma kwenye vituo
maalumu wakati wa Corona.
Picha
ya pamoja ya Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sellah
na Wauguzi na Wakunga wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mount Meru mara
baada ya kikao cha pamoja.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi
na Ukunga Bi. Ziada Sellah akizindua kitabu kinachoitwa “COVID-19 VITA
VYA KARNE YA 19” kilichoandikwa na Afisa Muuguzi Bi.Jane Barakululiza
ambaye ni mtumishi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa Mount Meru

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga akiongea na wauguzi wa hospitali hiyo
………………………………………………………………..
Na. WAMJW-Arusha
Wauguzi na wakunga nchini
wametakiwa kutumia lugha nzuri wanapokuwa wakiwahudumia wagonjwa kwani
kwa kufanya hivyo ni kinyume na maadili na miiko ya kazi yao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bi. Ziada Sellah wakati akiongea na Wauguzi waliopo wa
hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha-Mount Meru jijini hapa.
Bi. Ziada alisema kuwa wapo
baadhi ya wauguzi au wakunga hutumia lugha chafu kwa wagonjwa na mara
nyingine kuomba au kupokea pesa kutoka kwa wagonjwa pindi wanapofika
kupata huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
“Vitendo hivi ni kinyume na
maadili na miiko ya kazi yetu kwani katika viapo vya utumishi mliapa
kuwatumikia na kuwahudumia wagonjwa kwa moyo na upendo, hivyo
hakikisheni mnatimiza viapo vyenu”.Alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo, Bi. Ziada
aliwapongeza wauguzi wote kwa kupambana vyema katika janga la Covid-19
kwani kipindi kile walisimama mstari wa mbele na kupambana na ugonjwa
huo kwani ugonjwa huo ni mpya na hauna chanjo wala tiba.
“Niwapongeze sana kwa mapambano
dhidhi ya ugonjwa huo ambao uliikumba dunia na nchi yetu,licha ya
mazingira hatarishi lakini mliweza kupambana na hatimaye ugonjwa
kuondoka hapa nchini”.
Pia aliwataka wauguzi hao
kutambua thamani yao kwani wao ni askari wa mbele katika vita vyote
vya magonjwa kwa maana wao ndio wanampokea mgonjwa kwa mara ya kwanza
anapofika kituoni na kumuhudumia kipindi chote anapokuwepo hospitalini
hapo.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi
aliweza kuzindua kitabu kilichoitwa “COVID-19 VITA YA KARNE YA 19”
kilichoandikwa na Afisa Muuguzi Bi. Jane Barakululiza wa hospitali hiyo
ambacho kinaongelea maisha kipindi cha Corona na hata baada ya
Corona.Pia alitunuku zawadi kwa wauguzi waliopambana vyema katika
kupambana na ugonjwa wa Corona.
No comments :
Post a Comment