Meneja wa kitengo cha bidhaa za intaneti, Ndevonaeli Eliakimu, akiongea
na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma
mpya ambayo inampa mteja uwezo wa kurefusha muda wa matumizi ya
kifurushi ambacho kinakaribia kufikia ukomo wa muda wake wa matumizi.
Kushoto kwake ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisaeli Mapema leo
Jijini Dar es salaam.
“Sasa ni muda wa kuchukua kilicho chako na Tigo, okoa bando lako kabla ya muda wake kuisha” Woinde Shisaeli-Meneja mawasiliano Tigo #TigoChukuaKilichoChako
“Tigo tunahakikisha tunakuwa wa kwanza kumpatia mteja bidhaa& huduma ambayo ataifurahia kila wakati, Sasa tumekuja na huduma ya kipekee ‘Chukua kilicho Chako’ ambapo mteja anaweza kuokoa bando lake kabla ya kuisha” Woinde Shisael-Meneja mawasiliano Tigo #TigoChukuaKilichoChako |
· Huduma hii ya kurefusha muda wa matumizi wa vifurushi ni ya kwanza na ya aina yake nchini Tanzania
Dar es Salaam. 8 Septemba 2020. Kampuni
inayoongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano ya kidigitali nchini
Tanzania, Tigo, leo hii imezindua huduma mpya ambayo inampa mteja uwezo
wa kurefusha muda wa matumizi ya kifurushi ambacho kinakaribia kufikia
ukomo wa muda wake wa matumizi. Huduma hii mpya itawapa wateja fursa na
uwezo wa kuendelea kutumia kiasi cha kifurushi kilichobakia baada ya
kufikia kikomo cha muda awali wa matumizi. Hii itahusisha vifurushi vya
kupiga simu, kutuma meseji pamoja na data.
Huduma hii ya kuweza kurefusha muda wa matumizi kwa kifurushi kilichofikia kikomo cha muda wake wa matumizi maarufu kama ‘Chukua Kilicho Chako’ ni
ya kwanza na ya aina yake na kampuni ya Tigo ndiyo ya kwanza inayompa
uhakika mteja kuwa sasa hataweza kupoteza kifurushi chake ambacho
hakijatumika.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya, Meneja wa kitengo cha bidhaa za
intaneti, Ndevonaeli Eliakimu, amesema, “Kama mtandao wa kisasa wa
mawasiliano nchini Tanzania, tumewasikiliza na tumeamua kufanyia kazi
ombi hilo la wateja wetu ambao wamekuwa wakishindwa kutumia vifurushi
vyao kutokana na kuisha kwa muda wake wa matumizi. Hivyo basi huduma hii
mpya itawapa wateja uwezo wa kuongeza au kurefusha muda wa matumizi wa
vifurushi vyao kuanzia siku, wiki hata mwezi”.
“Kama
kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali na za
kisasa kabisa nchini Tanzania, tumekuwa wa kwanza kuzindua huduma hii
mpya na ya aina yake hivyo wateja wetu sasa hawatakuwa na wasiwasi juu
ya ukomo wa muda wa matumizi wa vifurushi vyao. Huduma hii inazidi
kudhihirisha namna Tigo inavyojidhatiti kuhakikisha inawathamini wateja
wake kwa kuwapatia huduma zenye ubunifu wa hali ya juu”, Eliakimu
ameongeza.
“Hivyo
basi kwa sasa vifurushi vitakuwa vinatumika kulingana na matakwa ya
mteja na hii pia inadhihirisha ushindi kwa wateja wote wa Tigo nchini
Tanzania na ni matumaini yetu kwamba huu ni mwendelezo wa kuboresha
huduma zetu ili kumrahisishia mteja wetu namna ya kuwasiliana na
wapendwa wake”, Eliakimu ameeleza.
Kupitia
huduma hii, mteja atapokea ujumbe kila kifurushi chake kitakapokaribia
kufikia mwisho wa muda wa matumizi, hivyo mteja ataweza kurefusha muda
wa matumizi wa kiasi cha kifurushi ambacho kimebaki ili aweze kuendelea
kukitumia mpaka kitakapokwisha.
No comments :
Post a Comment