Msaada wa vifaa zikiwemo runinga, taulo za kike, mipira na jezi kwa wasichana na wavulana.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la World Vision Tanzania Agnes John azungumza na vijana balehe katika utekelezaji wa mradi huo.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la World Vision Tanzania Agnes John azungumza na vijana balehe katika utekelezaji wa mradi huo.
Na Ismail Luhamba, Singida
Shirika World Vision Tanzania limetoa
vifaa mbalimbali vya elimu na michezo ikiwemo taulo za kike vyenye
thamani ya shilingi milioni 25, katika shule 14 za msingi na sekondari
zinazotekeleza mradi afya ya uzazi kwa vijana balehe katika wilaya za
Ikungi na Manyoni mkoni Singida.
Akikabidhi vifaa hivyo Mratibu wa
shirika World Vision Mwivano Malimbwi alisema lengo la kutoa vifaa hivyo
ni kuwasaidia vijana juu ya afya ya uzazi katika kupata elimu kupitia
mradi wao wa afya ya uzazi kwa vijana balehe.
"World Vision kupitia wafadhili wetu
tumetoa Televisheni katika shule za sekondari za
Kintandaa,Dungunyi,Iglansoni,Salanda pamoja na Nkonko,na tumetoa vifaa
vya michezo, taulo za kike katika shule za msingi na sekondari
tulizoziteua katika hizo halmashauri", alisema Malimbwi.
"Tumetoa hizi taulo za kike kwa
baadhi ya shule tulizoziteua kulingana na jiografia yake ya kuwa mbali
na huduma mbalimbali za kijamii ili ziwasaidie vijana wa kike
wanapoingia kwenye siku zao.nawaomba walimu wa hizo shule kuaandaa
maeneo ya kutupa hizo taulo baada ya kutumika kwa lengo la kutunza
mazingira",aliongeza
Malimbwi alieleza umuhumu wa
kushughulikia afya ya jinsia na uzazi kwa vijana ambapo amesema vijana
ni nguvu kazi na tegemeo katika uzalishaji mali,vijana ni
raslimali,hivyo wanahitaji kuboresha afya zao ikiwa ni pamoja na afya ya
uzazi ndio maana shirika hilo limekuja na program ya afya ya uzazi kwa
vijana balehe katika mikoa ya Singida na Shinyanga.
Akipokea vifaa hivyo afisa elimu mkoa wa
Singida kwa niaba ya katibu tawala mkoa Nelas Mlungu alilishukuru
shirika kwa msaada wa vifaa hivyo kama Tv ambazo zitawasaidia wanafunzi
hao kujifunza masuala ya afya ya uzazi.
Mlungu aliiomba jamii kusimamia malezi
na maadili yaliyobora kwa vijana na wasisubiri mashirika na wadau
wengine waje kusimamia masuala ya maadili.
"Tunawashukuru sana World Vision
Tanzania kwa msaada wenu na nawaomba walimu mkasimamie vifaa hivyo
visitumike vibaya bali vitumike kama ilivyotarajiwa", alisema Mlungu.
Hata hivyo walimu ambao shule zao
zimepata msaada huo waliwapongeza World Vision kwa msaada wa vifaa hivyo
kwani zitawasaidia watoto hao,na kwamba watahakikisha wanavitunza na
kutumika ipasavyo.
Wanafunzi shule za msingi na Sekondari
kutoka katika Wilaya ya Ikungi na Manyoni mkoani Singida, wakishiriki
michezo ikiwa ni sehemu ya mradi wa afya ya uzazi na lishe kwa vijana
balehe.
No comments :
Post a Comment