Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akifungua kongamano la Mawakala wa Benki ya CRDB kutoka Kanda ya Magharibi (wilaya ya Shinyanga,Kishapu na Nzega) lililolenga kujadili namna ya utoaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kidigitali .Kushoto ni Meneja Ufanisi Biashara Upande wa Mawakala kutoka Benki ya CRDB Makao makuu,Goodluck Ruhago akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui, kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney.
*****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi
imeendesha Kongamano la Mawakala wa Benki ya CRDB kwa ajili ya
kujadiliana kuhusu miongozo mbalimbali ya namna ya utoaji wa huduma za
kifedha kwa njia ya kidigitali ili kuongeza chachu ya kuongeza ufanisi
wa kazi,kuongeza umakini katika utoaji huduma za kifedha ili kukuza
vipato vyao.
Kongamano hilo la Mawakala wa Benki ya CRDB likiongozwa na Kampeni ya ‘CRDB Wakala… Ulipo tupo’
limefunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack leo
Jumanne Septemba 8,2020 na kuhudhuriwa na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB
na Mawakala wake takribani 300 kutoka wilaya ya Kishapu,Shinyanga na
Nzega.
Akizungumza wakati wa kufungua Kongamano
hilo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack aliipongeza Benki
ya CRDB kwa kuwa Benki inayoongoza kuwa na Mawakala wengi Tanzania na
kuwezesha Watanzania hasa waliopo katika fursa ya kilimo kupata huduma
za benki hasa maeneo ya vijijini.
“Kwenye maeneo ya kilimo haswa yale
mazao makubwa ya kimkakati mawakala wamesaidia kufungua akaunti za
wakulima ambao serikali inatumia kuwalipa wakulima kwa urahisi na
kutokana na ukaribu wa Wakala wa CRDB wakulima wanapata huduma wakati
wowote wanapohitaji kuweka na kutoa fedha,mfano wakulima wa zao la pamba
na tumbaku kwa kanda hii ya Magharibi”,alisema Telack.
“Pamoja na Benki ya CRDB kupanua
huduma za kibenki kupitia mawakala,tumeshuhudia kuongezeka kiwango cha
ajira kwa Watanzania wengi ambapo hadi sasa huduma ya Uwakala kupitia
Benki ya CRDB imeajiri takribani Watanzania 20,000 kutoka huduma ya
Wakala”,alisema.
Mkuu huyo aliwataka Mawakala wa Benki
kuchukua tahadhari na kujiepusha na matukio ya utakatishaji wa fedha kwa
kuwa ni rahisi zaidi kwa wahalifu kujaribu kuwatumia na kujiingiza
kwenye hasara ya biashara.
“Tunatambua Mawakala mnafanya kazi
nzuri,mmekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wafanyabiashara na wananchi kwa
ujumla kukamilisha miamala popote walipo na muda wowote pasipo kuogopa
hatari za biashara hiyo. Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya,niwasihi
kuchukua tahadhari kwa kufuata ushauri wa benki”,alisema Telack.
“Kuweni makini mnapofanya huduma za
kifedha,usimwamini mtu yeyote.Lindeni mitaji yenu,hatutaki kusikia
mnalizwa. Usimhudumie mteja bila kuhesabu fedha. Chukueni tahadhari
kwani mlinzi wa kwanza wa fedha zako ni wewe mwenyewe. Pia msijiingize
kwenye vitendo mikopo kinyume cha taratibu”,alisisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya
Magharibi Said Pamui alisema katika Kongamano hilo lilohudhuriwa pia na
Maafisa wabobezi wa masuala ya fedha kutoka CRDB Makao makuu,Mawakala
hao watafundiswa mbinu mbalimbali za kutambua ukatakatishaji wa fedha
ili waweze kuchukua tahadhari na kujiepusha na matukio ya utakatishaji
wa fedha.
Aidha Pamui alisema Mawala wa Benki ya
CRDB wamekuwa sehemu ya watoa huduma za fedha nchini Tanzania hivyo wana
mchango mkubwa katika kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapaa kiuchumi
hasa baada ya kufikia uchumi wa kati.
“Mawakala hawa katika utendaji wao wa
kazi lazima wahakikishe hawashiriki wala kusaidia vitendo vya
utakatishaji wa fedha kwani kila penye utakatishaji fedha uchumi
unadumaa”,alieleza Pamui.
“Na sisi benki ya CRDB kama
wawezeshaji wa Makawala wa Benki ya CRDB hatukubali kuwa sehemu ya
utakatishaji wa fedha ndiyo maana tumeandaa Kongamano hili ili kuwapa
mafunzo ya utoaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kidigitali ili watoe
huduma za fedha wakiwa wamebobea katika kutoa huduma za fedha kwa
umahiri mkubwa”,aliongeza.
Pamui alieleza kuwa Mawakala wa Benki ya
CRDB wamesaidia kuongeza muda wa utoaji huduma za kibenki kwa
wananchi,ambapo wapo wanaohudumia masaa 24, 18 na hata masaa 12 ambapo
ni zaidi ya masaa 8 ambayo matawi ya benki hutoa huduma.
Katika hatua nyingine Pamui aliwataka Mawakala hao kutoa elimu kwa wateja kuhusu umuhimu wa kutunza Nywila 'Password' za akaunti zao ili kuhakikisha fedha zao zinakuwa salama.
Kwa upande wake,Meneja Ufanisi Biashara
Upande wa Mawakala kutoka Benki ya CRDB Makao makuu,Goodluck Ruhago
alisema mpaka sasa kuna zaidi ya Mawakala 18,000 nchini,Benki
zinazotembea 15 na matawi ya Benki ya CRDB zaidi ya 250 na zaidi ya
asilimia 70 ya wateja wa Benki ya CRDB wanafanya miamala kupitia kwa
mawakala.
Katika Kongamano hilo, Benki ya CRDB imetoa zawadi kwa Mawakala 10 walioongoza kwa kutoa huduma bora ambapo Mshindi wa kwanza ni Idrop (T) Ltd amepata zawadi ya cheti na shilingi 200,000/=, mshindi wa pili Juliana Sebastian Shilatu, cheti na shilingi 100,000/=, mshindi wa tatu Mathew Albert Kihama, cheti na shilingi 75,000/=, mshindi wanne Benard Joseph Lewis, cheti na shilingi 50,000/= na mshindi wa tano Zaba General Supplies amepata zawadi ya cheti na shilingi 50,000=,
No comments :
Post a Comment