Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF),(pichani kati)
Lulu Ng’wanakilala, akifafanua jambo mbele ya Wageni waalikwa (hawapo
pichani kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika jana jijini Dodoma
Washiriki
mbalimbali wa kikao hicho wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa
yakiwasilishwa na baadhai ya Wajumbe wa kikao hicho ndani ya jiji la
Dodoma
Meneja
Mawasiliano wa LSF, Jane Matinde akizungumza jambo mbele ya wageni
waalikwa katika kikao kazi hicho kilichofanyika ndani ya jiji la Dodoma.
NA HAMIDA RAMADHANI-CPC DODOMA.
JAMII
imetakiwa kuacha uoga na badala yake imeaswa kuwatumia wasaidizi wa
msaada wa kisheria hasa wanawake pale wanapo kandamizwa kwenye suala
zima la haki zao za msingi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jana,Afisa Ufuatiliaji Tathimini Hamisa Hamad
kutoka Pemba kwenye kikao cha tathimini amesema lengo la kikao ni
kufanya mapitio ya mambo ambayo tumeyatelekeza ndani ya mwaka.
Katika
kikaokazi hiki tunatekeleza mapitio tuliyoyafanya ndani ya mwaka mmoja
na Kama inavyojulikana kwa sisi upande wa Zanzibar msaada wa kisheria
ulikua mgeni kwetu kutokana na mila na desturi na dini.Hamisa Hamad
Amesema
Msaada wa kisheria kwa Zanzibar ilikua ni kitu kigeni kutokana na mila
na desturi na dini lakini baada ya kufika mwaka 2007 baada ya shirika la
Legal services facility LSF)kufika ndipo wanawake 850 waliamka na
kuanza kutoa taarifa za kikatili wanazo fanyiwa na wenza wao na kupatiwa
msaada wa kisheria.
“Zamani
kwa sisi Awaafrika kwa mila zetu na deaturi ilikua ni ngumu kutoka
kwenda kumshitaki mwenza wao eti tu kwakukosea au kwakufanyia tendo la
ukatili hali iliopelekea sisi wasaidizi wa kisheria kukosa takwimu
sahihi za kuwatambua ni wanawake wangapi waliofanyiwa ukatili wa
kijinsia”amesema Msaidizi wa kisheria Hamisa
Aidha amesema katika mila za kiafrika wanawake na watoto ndio wanaongoza kwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia.
MAFANIKIO.
Amesema
baada ya kuja kwa wasaidizi wa msaada wa kisheria wanawake wengi
wamejitokeza na kuanza kudai haki zao za msingi ikiwemo kudai ardhi
,asilimia 99 ya wanzanzibar ni waislam.
Amesema
katika dini ya kiislam imeainisha wazi mwanamke akifa anatakaiwa apewe
haki zake kadhaa na mwanaume haki kadhaa lakini jambo hilo limekuwa
likikiukwa na wanaume wamekua wakiwakandamiza.
“Sasa
ni vyema wanawake wote kujitokeza katika kudai haki zao kwani mwanamke
ana haki zake ya kutunzwa kupewa mirathi na ikitokea umeachwa dai haki
zako na kama ikitokea hata mwaume amefariki mwanamke anatakiwa apewe
haki zakezote “amesema Msaidizi wa kisheria Hamisa
Naye
Afisa Ufuatiliaji na Tathimini kutoka mkoani Lindi Nelson Choaji
amesema kazi yao kubwa katika mkoa wa lindi ni kuhakikisha upatikanaji
wa haki katika mkoa wa Lindi unapatikana.
Hata
hivyo amesema kwa upande wa Lindi Legal Service Facility imekua ikiwapa
nguvu wasaidizi wa kisheria kuhakikisha wanawafikia watu wote wenye
changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo katika jamii.
Tatizo
kubwa la mikoa ya pwani kesi nyingi tunazokumbana nazo ni za wanaume
kutekeleza familia zao mi nitoe wito tu kwa kina mama kuwatafuta
wasaidizi wa msaada wa kisheria pindi wanapo hitaji haki zao za msingi.
Nelson Choaji
Legal
Service Facility ni Shirika lisilo la kiserikali lenye makao Makao
Makuu yake jijini Dar es salaam lengo kuu la uanzishwaji wake ni
kusaidia jamii kupata haki.
No comments :
Post a Comment