Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Brigedia Generali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Mratibu Mkazi
wa Umoja wa Mataifa nchini,
Bw. Zlatan Milišić alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 2 Septemba 2020.
Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo
Balozi Ibuge alitoa shukrani kwa Shirika hilo kwa ushirikiano uliopo
kati yake na Serikali hususan kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya
kiuchumi na kijamii. Kwa upande wake, Bw. Milišić aliipongeza
Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu ambao ni chanzo cha uchumi wa
nchi kustawi. Pia aliipongeza kwa kuendelea kuchangia vikosi vya ulinzi
wa amani kwenye mataifa mbalimbali yenye migogoro duniani na kuitakia
Tanzania uchaguzi wa amani na utulivu hapo mwezi Oktoba 2020. |
No comments :
Post a Comment