Afisa
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UmojaSwitch Ndugu Danford Mbilinyi (
Kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Ndugu Magesa
Wandwi, kwa pamoja wakisaini Mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa
kibiashara kati ya Halopesa na UmojaSwitch. Akishuhudia Kulia ni Afisa
mawasiliano Halotel Bi. Hindu Kanyamala na Kushoto ni Bi. Adellah
Kaihula Afisa Masoko wa UmojaSwitch.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Ndugu Magesa Wandwi (kulia)
akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kutoa
pesa kwenye ATM za Umoja katika makao makuu ya Ofisi za Halotel Dar es
salaam,alisema Huduma hiyo itawawezesha wateja wote wa Halopesa kutoa
pesa kupitia ATM zote za Umoja. Kushoto ni Afisa Mkurugenzi Mkuu wa
UmojaSwitch Ndugu. Danford Mbilinyi.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Ndugu Magesa Wandwi (kulia)
na Afisa Mkurugenzi Mkuu wa UmojaSwitch Ndugu. Danford Mbilinyi
,wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara kati
ya Halopesa na UmojaSwitch, ambapo wateja wa Halopesa nchini wataweza
sasa kutoa Pesa katika ATM za umoja zilizopo katika maeneo mbalimbali
hapa nchini.Afisa
bidhaa na masoko wa Halopesa, Bi.Roxana Kardio akitoa maelekezo jinsi
ya kutoa pesa kwenye ATM za Umoja katika mojawapo ya ATM za umoja jijini
Dar es Salaam.
*************************************
Taarifa kwa vyombo vya Habari.
Dar es Salaam, 02 Septemba, 2020, Kutokana na kasi ya ukuaji wa
teknolojia na uchumi, Halopesa imeendelea kutanua wigo wa kutoa huduma
zake za kifedha nchini ikizingatia pia
mkakati wa kitaifa wa
ujumuishwaji wa wananchi katika matumizi ya mifumo rasmi ya kifedha
chini.
Ikiwa ni mwendelezo wa kuwafikia na kuwapa wateja wa Halopesa
huduma bora kwa urahisi na uhakika, Halotel kupitia Huduma yake ya
HaloPesa imeingia ubia na Kampuni ya UmojaSwitch kutoa huduma kwa wateja
wa HaloPesa ya kutoa fedha kupitia ATM za Umoja zilizoko kote nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hii katika ofisi za Makao
Makuu ya Halotel, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa Ndugu ,
Magesa Wandwi, amesema kuwa ni hamasa na lengo letu kuhakikisha kuwa
tunaendelea kutumia miundo mbinu ya teknolojia na fursa zote zilizopo
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta hii ya huduma za
kifedha na kuwapa wateja wetu huduma bora na za uhakika na nifuraha yetu
leo kushirikiana na UmojaSwitch kuzindua rasmi huduma hii ambayo
itawawezesha wateja wa HaloPesa kutoa fedha kwa urahisi na uhakika zaidi
kupitia ATM za Umoja zaidi ya 250 zilizopo maeneo mbalimbali kote
nchini.
Tunapenda kuwasisitizia wateja wetu kuwa Huduma hii haitakuwa na
makato ya ziada tofauti na makato ya kawaida ya kutoa pesa kwa wakala
wa kawaida, lakini pia huduma hii haitahusisha matumizi ya internet pale
ambapo mteja atakuwa anatoa fedha kwenye ATM za Umoja, aliongeza
Magesa.
Kwa Huduma hii pamoja na mawakala wetu zaidi ya Elfu Hamsini
(50,000) waliosambaa nchini kote kwa pamoja tutaendelea kuwahudumia
wateja wetu wa Halopesa zaidi ya Milioni Mbili (2,000,000) waliopo
mijini na vijijini.
Mteja wa Halopesa atapitia hatua za kawaida kutoa pesa kwa
kupiga *150*88# kisha kuchagua ‘2’, (Kutoa Pesa ), Kisha chagua tena “2”
(UmojaATM), ataendelea na kuweka kiasi na namba yake ya siri ya
Halopesa, baada ya hapo atapata ujumbe wenye namba ya siri ya
uthibitisho ambayo ataitumia kutoa fedha katika ATM za Umoja. Aliongeza
Magesa.
Akiongea na waandishi wa Habari katika uzinduzi huo, Mkurugenzi
mkuu wa UmojaSwitch, Ndugu. Danford Mbilinyi, alisema ushirikiano na
Halopesa utaongeza upatikani wa huduma za kifedha kirahisi nchini
kupitia ATM zetu zaidi ya 250 zilizoenea nchi nzima na kwamba wateja wa
HaloPesa wana fursa nyingine ya uhakika sasa ya kupata fedha muda wowote
mahali popote nchini.
No comments :
Post a Comment