Mgeni
Rasmi katika hafla ya makabidhiano ya miradi ya vyoo na maji kati ya
shirika la World Vision Tanzania na serikali Katibu tawala mkoa wa
Kagera Prof. Faustine Kamuzora watatu kutoka kushoto akikata utepe
kuashiria kuzindua matumizi ya maji.
Prof. Faustine Kamuzora katibu tawala Mkoa wa Kagera wa kwanza kushoto
akipokea mradi wa vyoo kutoka kwa Juliana Charles meneja wa World Vision
Kanda ya Kagera kulia baada ya kukamilika kwa mradi huo.
Muonekano
wa vyoo katika shule ya msingi Biyungu na Kiruruma wilayani Karagwe
walivyokuwa wakitumia wananfunzi wa shule hizo kabla ya shirika la World
Vision kujenga vyoo vipya.
Muonekano wa vyoo
vilivyojengwa na shirika la World Vision Tanzania Mradi wa Bushangaro
AP katika shule za Biyungu na Kiruruma wilayani Karagwe Kagera.
Katibu
tawala Prof. Faustine Kamuzora akiwa na viongozi wa shirika la World
Vision Tanzania pamoja na kamati ya maji kwenye chanzo chan maji
kilichojengwa na World Vision Tanzania kwa gharama ya shilingi milioni
400.
***************************************
Na Allawi Kaboyo Karagwe.
Shule za
msingi za Biyungu na Kilruruma wilayani Karagwe Mkoani Kagera ni
miongoni mwa
shule zilizokuwa na changamoto kubwa ya vyoo vya wananfunzi
kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wananfunzi licha yakuwa shiri la
World Vision kuasaidia katika sekta hiyo.
Katika hafla
ya kukabidhi matundu manane ya vyoo kwa kila shule yaliyojengwa na
shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania Mradi wa
Bushangaro AP kwa serikali ya mkoa,meneja wa shirika hilo kanda ya
Kagera Juliana Charles amesema kuwa walifika katika shule hizo na
kusikitishwa na hali waliyoikuta na kuwiwa kuanzisha ujenzi wa vyoo
hivyo.
Juliana
amesema kuwa shirika hilo linajihusisha Zaidi na makuzi ya mtoto hivyo
kujenga miundombinu ya vyoo mashuleni ni moja ya huduma muhimu kwa mtoto
ambayo itampelekea kusoma kwa raha lakini pia kuweza kumuepusha na
magonjwa mbali mbali ya mlipuko yanayoweza kumtokea.
Sambamba na
ujenzi wa vyoo hivyo shirika hilo pia limekabidhi mradi wa maji ambayo
mtandao wake umesambazwa kwenye vijiji viwili ambavyo vipo kata ya
Bushangaro na kuweza kusambazwa katika zahanati ya Nyakagoyagoye ili
kuweza kurahisisha huduma hiyo kwa jamii ya wanakaragwe.
Katibu Tawala
wa mkoa Kagera Profesa Faustine Kamzora baada ya kukabidhiwa miradi
hiyo ameitaka jamii kuitunza miradi na kutunza mazingira ili kuhakikisha
ubora wa miradi unabaki ulele ule ambapo pia ameutaka uongozi
utakaosiamamia mradi wa maji kuhakikisha maji hayo wanayatibu kabla ya
kumfikia mwananchi ili kumuepusha na magonjwa.
Kamzora
amesema mradi umejingwa kwa ufadhili wa nchi ya Ujerumani kwa garama ya
zaidi ya shilingi milioni 400 na endapo Mazingira ya miundomibun ya
maji yakiwekwa kwenye hali ya usafi unao zingatia matunzo bora
unaweza kuondoa magonjwa yanatokana na matumbo hasa kwa watoto wadogo.
Aidha Kamzora
almesema,vituo vya afya na Hospitali na zahanati kwa asilimia kubwa
zinapokea matatizo ya magonjwa ya upungufu wa maji kwa asilimia 70
pamoja nna magonjwa ya tumbo kutokana na watu kutumia maji ambayo sio
salama ambayo yote hayo ni ukosefu na uhaba wa maji yenye uhakika .
“ pia
maji yanafaida nyingi na sio kuondoa magonjwa ya tumbo na upungufu wa
maji mwili pekee bali na kuanzisha bustani majumbani na kujipatia lishe
bora ya watoto lakini pia matumizi mengine ya nyumbani ikiwemo kufua
na kufanyia usafi mwingine”amesema Kamzora.
Meneja wa
shirika la Worldvision kanda ya Kagera Juliana Charles amesema mradi
huo utahudumia wananchi ambao awali walikuwa wakitumia muda mrefu
kufuata maji vijiji jirani ambayo bado yalikuwa hayapo katika usalama.
Charles amesema kuwa,”baada
ya kupatiwa taarifa na kamati ya maji kijijini hapo, shirika liliweza
kufika eneo la chanzo na kufanya tathimini ya shughuli ya ujenzi
utakaoweza kuzua mifugo isiweze kuingia ndani ya maji hayo kwa
kuyazumguzisha, .
Shirika
limefanya ujenzi wa chanzo kwa kujengea maji ikiwa ni kuzuia mifugo,na
kutunza chanzo kisiweze kuharibiwa na jamii ambayo inatakiwa yenywe
itunze chazo hiki”.
Mwenyekiti wa
kjiji cha Nyakagoyagoye Salmoni Mtilani alisema, kukamilika kwa ujenzi
huo utaondoa watoto kutumia muda mwingi kutafuta maji na wakati
mwingine kutokuhudhulia shuleni kwa ajiri wazazi wao kuwatuma maji
umbari mrefu
“ Sio
watoto sio wazazi wao wanatembea umbari mrefu wa kilomita18 kwenda
kijiji jirani kufuata maji ambayo hayachangamani na mifugo kijingine
watoto kutohudhulia shuleni kabisa na kuwafanya kukosa masomo na
hatimaye kushuka kitaaluma” Amesisitiza Mtilani
No comments :
Post a Comment