Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy
Mwaluko, akifungua warsha ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma
iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji
ya Mwaka 1996, leo tarehe 11 Jijini Dodoma, kikao kazi hicho
kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi akieleza umuhimu wa wadau kuidhinisha
taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,
wakati wa kikao kazi ikilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo
tarehe 11 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa warsha
ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi
kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya
Uwekezaji ya Mwaka 1996, warsha hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa warsha
ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi
kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya
Uwekezaji ya Mwaka 1996, warsha hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Jumanne Gomera, akiwasilisha wasilisho la taarifa
ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, wakati
wa warsha ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma kujadili taarifa hiyo,
kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11
Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi
cha wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia Warsha iliyolenga
kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka
1996, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe
11 Jijini Dodoma.
Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi na Mtaalamu
wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar
es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje wakiteta jambo wakati wa kikao kazi cha
wadau wa uwekezaji sekta ya Umma iliyolenga kuidhinisha taarifa ya
Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, kikao kazi hicho
kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
**************************************
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara
ya Maendeleo ya Uwekezaji imekutana na wadau wa uwekezaji wa sekta ya
Umma kwa lengo la kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa
Sera
ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996. Wadau hao ni kutoka Wizara, Idara,
Taasisi na Wakala wa Serikali. Baada ya kupokea taarifa ya Tathmini ya
Utekelezaji wa Sera hiyo,wameridhishwa kwa jinsi ilivyobainisha nchi
inavyoweza kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji ili kuvutia
uwekezaji wa ndani na nje.
Wakipongeza wakati wa kujadili
taarifa hiyo, leo tarehe 11 Septemba, 2020 jijini Dodoma. Wadau hao
wamesisitiza Tathmini hiyo iliyojikita kwenye masuala ya kisera,
kisheria na kiutendaji inaendelea kutoa mapendekezo ya kuendelea kutatua
changamoto za uwekezaji nchini hususani kwenye maeneo ya Uratibu wa
Masuala ya Uwekezaji, Utangazaji wa Fursa za Uwekezaji, Uwezeshaji
Uwekezaji, pamoja na Vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi.
Akiongea wakati akifungua kikao
kazi hicho, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Uwekezaji), Bibi Dorothy Mwaluko amesisitiza kuwa upo umuhimu wa wadau
hao kubainisha masuala ya kisera, kiutendaji na kisheria, ili
kuhakikisha kuwa Sera ya Taifa ya uwekezaji na Sheria ya Uwekezaji
nchini haikinzani na sheria nyingine za kisekta kwenye masuala ya
uwekezaji.
“Serikali imekuwa ikitunga Sera
na Sheria kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara
nchini, tunahitaji kuwa na Sera madhubuti za kuvutia na kuwezesha
uwekezaji katika sekta zote ili kutumia vilivyo fursa za uwekezaji
zinazopatikana nchini.”Amesisitiza Mwaluko.
Akiongea kwenye kikao kazi hicho
Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje, amefafanua kuwa kukutana kwa
wadau hao kujadili taarifa ya tathmini hiyo kutawezesha kujua changamoto
wanazozipata wakati wa utekelezaji wa sera hiyo na hatimaye utatuzi
wake, utawezesha uwekezaji na kuleta tija kwa mwananchi wa kawaida.
Naye Mkurugenzi wa Uwezeshaji
Uwekezaji, kutoka Mamlaka ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (EPZ), James
Maziku amefafanua kuwa, sera hiyo imetungwa kwa muda mrefu hivyo
tathmini hiyo itasaidia kuhuisha (Review) Sera na Sheria za uwekezaji za
kisekta, kupunguza migongano ya kiutendaji na kuelewa namna ya
kuboresha utendaji wa pamoja wa kisekta.
Sera ya Taifa ya Uwekezaji
imebainisha malengo mahsusi sita (6) na malengo nane (8) ya kisekta.
Baadhi ya malengo hayo ni kuhamasisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa kwa
ajili ya mauzo ya nje; Kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi; Kuhimiza na
kuvutia matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwekezaji; Kuweka mfumo
mzuri na wa wazi wa kisheria; na kuondoa urasimu katika taratibu za
upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.
Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya
Mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997 iliyoanzisha Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC), vinaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
kushirikiana na Wizara za kisekta, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Kituo cha Uwekezaji Tanzania
kimepewa jukumu la kuratibu, kuvutia, kutangaza na kuwezesha wawekezaji
hapa nchini.
No comments :
Post a Comment