Katibu
Mtendani wa TCU , Profesa Charles Kihampa akizungumza wakati wa
uzinduzi wa maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Septemba 2, 2020.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,
akizungumza na kufungua Maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yanayifanyika katia
viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, leo Septemba 2, 2020
Mwenyekiti
wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Profesa Mayunga Nkunya akizungumza wakati
wa uzinduzi wa maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Septemba 2, 2020
Viongozi Mbalimbali wakitembelea mabanda katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika jijini.
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo,
ametoa wito kwa vyuo vikuu na taasisi za utafiti kujielekeza zaidi
katika kufanya tafiti zenye lengo la kujenga msingi wa uchumi wa viwanda
.
Dk.
Akwilapo amesema hayo Leo Septemba 2,2020 wakati akifungua maonesho ya
15 ya vyuo vikuu nchini yanayoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
(TCU), ambapo vyuo mbambali vimeshiriki maonesho hayo.
Amesema
taasisi hizo za utafiti zinatakiwa zifanye utafiti katika maeneo
mbalimbali, hususani utafiti wa madini, utalii,uvuvi, Kilimo, mifugo,
teknolojia, maliasili za misitu na bidhaa za viwandani.
Aidha,
amesema hadi sasa Serikali imeshatoa Sh. Trilioni 1.03 kwa ajili ya
kugharamikia elimu bure ya msingi, ambapo hali hiyo imesababisha
wanafunzi kuongezeka.
"Elimu
hii bure imesababisha wanafunzi kuongeza kwa kasi kubwa kutoka Milioni
8.3 mwaka 2015 hadi kufikia milioni 10.9 mwaka huu, kwa hali hii vyuo
vikuu vinatakiwa kupanua udahili wa wanafunzi," amesema Dk.Akwilapo
Katibu
huyo, amesema udahili huo ukishatanuliwa utaweza kumudu idadi ya
wahitimu watakaomaliza elimu ya bila malipo ngazi ya msingi na Sekondari
kwa siku zijazo.
"Idadi
ya wanafunzi wa kitado cha kwanza hadi cha nne nayo imeongezeka kutoka
Milioni 1.6, 2015 hadi kufikia Milioni 2.2 mwaka 2019, huku kidato cha
sita wakiwa 153,000, ,"
"Kutokana
na idadi hii tunatambua kuwa kutakuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi
watakaomaliza elimu ya Sekondari na kuingia vyuo vikuu, hivyo vyuo
vinapaswa kuangalia namna ambavyo vitapanua udahili ili kuweza kumudu
idadi hii," amesema
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa TCU, Profesa Mayunga Nkunya amesema tume hiyo
imeendelea kushirikiana vyuo vikuu kwa kuvishauri vitoe elimu na
kuandaa mitaala inayoendana na vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa.
Pia, amesema tume hiyo imeimarisha mifumo yake ya utoaji elimu kwa umma na hivyo kuweza kuwafikia wadau wengi zaidi.
"Kwa mara ya kwanza tume imeweza kusajili jumla ya kampuni 14 zinazohusika na udahili wa wanafunzi,
lengo la usajili huu ni kuwalinda watanzania wanaokwenda kusoma nje ya nchi dhidi ya mawakala wasio waaminifu," amesema
Amesema
TCU imeendelea kutekeleza majukumu yake ya kuwatumikia watanzania
katika sekta hiyo ya elimu ya juu ili kuhakikisha wanapata elimu yenye
kukidhi viwango vya ubora vya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Naye,
Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema katika maonesho
hayo jumla ya taasisi 67 zimeshiriki na kuongeza kuwa kati ya hizo 58 ni
zile zinazotoa elimu ya juu.
No comments :
Post a Comment