Afisa
Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi pamoja na utoaji
wa elimu wa wananchi wanaotembelea Banda hilo katika maonesho ya 15 ya
vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU)
yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Afisa
Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu walivyojipanga katika ukaguzi wa viwango wa
vitabu vya hesabu katika sekta binafsi na sekta za umma katika maonesho
ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU)
yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Mzee
Joseph Temba akisoma moja ya kitabu cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) alipotembelea banda la Bodi hiyo
katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu
nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es
Salaam.
Afisa
Utafiti kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu
Tanzania(NBAA), Michael Mwakifuna akimsikiliza Bahati Gewye mara baada
ya Afisa wa NBAA kimfafanulia muundo wa mitihani ya Bodi alipotembelea
banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)
katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo
Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar Es Salaam.
Afisa
Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, Bertha Kipangula(kulia) akitoa ufafanuzi
kuhusu ufanyaji wa mitihani ya Bodi kwa Koneleth Herzon na Devoth Mateni
walipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu
Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na
Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Afisa
Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka (kulia) akitoa
ufafanuzi kuhusu ufanyaji wa mitihani ya Bodi pamoja na ada zinazotolewa
na Bodi hiyo kwa wananchi waliotembelea banda la Bodi ya Taifa ya
Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 15 ya vyuo
vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu jijini Dar
es Salaam, Afisa Masoko na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Magreth Kageya
amesema ni kosa kwa baadhi ya Vikundi, Taasisi kuajiri watu na kuwapa
vyeo vya Uhasibu na Ukaguzi.
Kageya amesema
hairuhusiwi watu kupewa vyeo hivyo bila kupita ngazi maalum katika Bodi
hiyo sambamba na kufikia ngazi ya CPA, ameshauri Taasisi, Mashirika hayo
kuuliza kwa Bodi hiyo ni mtu wa aina gani anapaswa kuwa Mhasibu au
Mkaguzi.
Kwa upande wake, Afisa Mdhibiti wa
Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka amesema Bodi hiyo kwa sasa ina
Kitengo cha (Member Service) ambapo chini yake kuna Audit Quality Review
(AQR) ambayo inahusika kukagua kuhakikisha Kaguzi zinafanyika kwa
mujibu wa sheria za nchi na kukidhi viwango vya Kimataifa.
Hata
hivyo, Bodi hiyo imeanzisha Mfumo wa usajili kwa Wanafunzi na Wanachama
kwa njia ya mtandao, sambamba na usajili wa mitihani ya Bodi na
kusajiliwa kwa Wanachama kupitia tovuti ya Bodi hiyo amabyo ni www.nbaa.go.tz.
No comments :
Post a Comment