Wanafunzi
wa shule ya awali na msingi ya Baobab iliyoko Mapinga Bagamoyo
wakionyesha umahiri wa kucheza nyimbo mbalimbali za asili katika bonanza
la aina yake lililofanyika shuleni hapo kwaajili ya kuibua vipaji.
Wanafunzi
wa shule ya awali na msingi ya Baobab iliyoko Mapinga Bagamoyo
wakionyesha umahiri wa kucheza nyimbo mbalimbali za asili katika bonanza
la aina yake lililofanyika shuleni hapo kwaaajili ya kuibua vipaji.
Wanafunzi
wa shule ya awali na msingi ya Baobab iliyoko Mapinga Bagamoyo
wakionyesha mitindo ya mavazi kwenye bonanza lililoandaliwa na shule
hiyo kwaajili ya kuibua vipaji vya wanafunzi.
======== ========
WANAFUNZI
wa Shule ya Msingi na Awali ya Babobab ya Mapinga Bagamoyo, wametia
fora kwenye bonanza ambapo wameonyesha vipaji vya aina mbalimbali.
Katika
bonanza hilo lililowashirikisha wanafunzi wa shule ya awali na msingi,
wanafunzi hao walionyesha umahiri kwenye kuigiza michezi mbalimbali
ikiwemo ile ya maonyesho ya mavazi.
Miongoni
mwa vitu vilivyotia fora kwenye bonanza hilo ni mitindo mbalimbali ya
mavazi iliyoonyeshwa na wanafunzi hao na namna walivyomudu kuwasilisha
sanaa hiyo kwa ubunifu mkubwa.
Mkuu
wa shule hiyo, Ireneus Njelekela alisema waliandaa bonanza hilo kwaajili
ya kuendeleza vipaji vya wanafunzi hao kwenye fani mbalimbali.
Alisema
mbali na masomo ya darasani shule imeona umuhimu wa kuwakutanisha
wanafunzi hao kwenye bonanza ili waonyeshe vipaji walivyonavyo kwenye
mitindo ya mavazi, muziki wa bongo fleva na maonyesho ya mitindo ya
mavazi.
Alisema
watakuwa wakiandaa bonanza kama hilo kila miezi mitatu kwaaajili ya
kuvumbua vipaji na kuvile kwani vinaweza kukua na kuwanufaisha kwenye
maisha yao ya baadaye.
“Mbali
na masomo ya darasani tumeona kuna umuhimu wa kubaini vipaji vya
wanafunzi na kuvikuza mtoto lazima alelewe katika Nyanja mbalimbali
kwasababu mwisho wa siku anawez kuishi kutegemee kipaji chake,” alisema
“Kuna
mifano ya wanamuziki wengi ambao wamefanikiwa sana kwenye maisha
kutokana na vipaji mbalimbali, mwanafunzi anaweza asifany vizuri sana
darasani lakini akawa na kipaji kitakachompa maisha mazuri sana,”
alisema
No comments :
Post a Comment