Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania Jean Francoius
akiangalia mfumo wa Oil katika gari iliyopita kupata huduma wakati
uzinduzi ampapo mwenye gari amepata kuwekewa mafuta bure na kuwekewa
Oil.
Mkurugenzi
wa Ushirikiano wa Kampuni Marsha Msuya-Kilewo akizungumza namna
wanavyoingia Ubia na watanzania katika umiliki wa vituo vya nishati ya
mafuta wakati uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Total Mchigani Goba
jijini Dar es Salaam.
Mmiliki
wa Kituo cha Mafuta Total Mchigani Goba Mhandisi Frank Malle
akizungumza kuhusiana namna alivyowezeshwa na Kampuni ya Mafuta Total
kumiliki kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
Mliliki
wa Kituo cha mafuta cha Total Mchigani Goba Mhandisi Frank Malle akiwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Jean Francois wakikata utepe kuashilia
uzinduzi wa kituo hicho jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Total wakiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Kituo
cha Mafuta na baadhi ya wgeni waalikwa katika uzinduzi huo,jijini Dar es
Salaam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Kampuni
ya Mafuta ya Tatal imesema kuwa iko katika mikakati ya kuwawezesha
Watanzania umiliki wa vituo vya mafuta katika maeneo ambayo yanaweza
kufanya biashara hiyo kwa kuwawezesha kufanya biashara .
Mkakati
wa kuwawezesha watanzania kumiliki vituo vya mafuta unahitaji
watanzania 100 lakini hadi sasa ni watanzania Nane wamewezeshwa kuwa na
vituo vya mafuta kwa kigezo kuwa na ardhi pamoja na mwenye ardhi
kuwekeza katika ujenzi.
Akizungumza
wakati wakati wa uzinduzi kituo cha mafuta cha Mchigani Goba jijini
Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Total
Tanzania Jean Francoius amesema kuwa Mmilki wa Kituo cha mafuta hicho
Mhandisi Frank Malle amepata katika mfumo wa DODO ambao kampuni imekuja
nao katika kuhakikisha watanzania wanakuwa sehemu ya kumiliki vituo vya
mafuta.
DODO
ni mfumo wa kibiashara ni mfumo wa kibiashara ambao kampuni ya Total
kutumia katika kuongeza mtandao vituo vya nishati ya mafuta nchini
unaowezesha wafanyabiashara kuingia katika mfumo wa ubia na kuweza
kumilki ,kuendesha pamoja na kusimamia vituo vya huduma ya mafuta vyenye
chapa ya Total.
Amesema
kuwa wameweka kituo hicho ikiwa ni kuhakikisha wananchi wa Goba
wanapata mafuta yenye kiwango bora na vilainishi bila kusahau basi za
kubeba abiria zinazotumia barabara ya Goba katika safari za Mbezi Mwisho
,Tegeta pamoja na Kimara.
Francocius
amesema kuwa Kampuni ya Total wanauzoefu wa biashara ya nishati ya
mafuta nchini zaidi ya miaka 50 ikiwa na mtandao nchi nzima na kuwa
na vituo vya Total pekee unaoweza kupata mafuta yenye excellium yenye
uwezo wa kusafisha injini pamoja na oli kutoka kwa wataalam wabobevu
waliotayari kutoa huduma.
Nae
Mmiliki wa Kituo cha Mafuta Frank Malle amesema kuwa katika maisha yake
hajawahi kufikiria kufanya biashara ya mafuta lakini Total imemwezesha
kuwa miongoni mwa watazania wanaomiliki vituo vya mafuta.
Amesema
wazo hilo lilikuja kutokana na ardhi aliyeinunua kwa ajili ya makazi
zilitokea kampuni nne za mafuta zikitaka eneo kisha kwenda Total na
kuweza kuingia kupata utalaam na kuwezeshwa umiliki huo.
Malle
amesema anawashukuru Total kwa uwezeshaji wa kuwa na kituo cha mafuta na
kuahidi kuendelea kufanya biashara hiyo kwa kuongeza vituo vingine.
Nae
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kampuni Marsha Msuya-Kilewo amesema kuwa
wanaendelea na mkakati wa kuweza kufika vituo 100 vya mafuta kwa
watazania kumiliki ambapo hadi sasa ni vituo Nane tu.
No comments :
Post a Comment