Mkuu
wa Chuo cha Maendeleo ya Mipango Vijijini Profesa Hozen Mayaya
akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ushiriki wa maonesho ya vuo
vikuu yanayofanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja.
Msajili
wa Wanafunzi Profesa Mirabless Malila akitoa maelezo namna wanavyotoa
elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwa wahadhili wabobevu katika Nyanja ya
mipango.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
CHUO
cha Maendeleo ya Mipango Vijijini Dodoma kimesema maendeleo yeyote ili
yaweze kutokea kunahitaji kuwepo kwa mipango hivyo I chuo pekee
kilichojikita katika kutoa elimu katika eneo hilo
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu jijini Dar es
Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa Hozen Mayaya amesema kuwa katika
maonesho ni kuleta wanafunzi pamoja kusoma elimu iliyojikita kusukuma
maendeleo ya nchi katika uandaji wa mipango.
Amesema
wamekuwa na kozi za muda mrefu na kozi za muda mfupi ambapo wanafunzi
wakihitimu wanaweza kuendelea na shahada katika kuongeza uwigo kuwa
mwanataaluma bora katika mipango na hadi shahada ya uzamivu.
Mayaya
amesema kuwa katika eneo lingine walilojikita ni pamoja na kutoa
ushauri ambapo katika ushauri huo kwa kushirikiana na UNDP wanajenga
kiwanda cha kutengeneza Barafu kanda ya Ziwa katika kuchochea mandeleo
ya uvuvi wa samaki kwa kuhakikisha samaki hawaozi.
Hata
hivyo amesema kuwa katika kutoa elimu pia wanafanya utafiti mbalimbali
wa kuweza kuwasaidia watanzania kuondokana na umasikini katika maeneio
mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo na maeneo waliyofanya katika wilaya
Mbulu kumekuwa na matokeo chanya ya kilimo cha vitunguu Swaum.
Profesa
Mayaya amesema kuwa katika utoaji wa elimu nchini wanampongeza Rais
Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuifikisha nchi katika Uchumi wa kati kwa
muda ambao haukutarajia kufika kama nchi.
Aidha
amewataka wazazi na wanafunzi kusoma Chuo hicho ili kuweza kuja
kuisaidia nchi katika upangaji wa maedeleo na hatimaye nchi kwenda
kwenda uchumi wa juu zaidi kwa kushirikiana na viongozi wa wa nchi.
Mkuu
wa Chuo Profesa Mayaya amesema katika maonesho yajayo watakuja na
matokeo ya taifiti kama serikali ilivyoagiza ili kuonyesha uhalisia wa
vitu wanavyofanya katka chuo hicho.
No comments :
Post a Comment