Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe , Profesa Lugano Kusiluka akipata maelezo
alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 15 ya Vyuo
Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Rose
Joseph.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka akizungumza alipotembelea
banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu
yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Rose
Joseph.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka akizungumza na Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi alipotembelea
banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu
yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Wafanyakazi
wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiwadahili wanafunzi katika maonesho ya vyuo
Vikuu yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wa kwanza kushoto akiwa na viongozi mbalimbali katika maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu yanayoendele kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi
wa akipata maelezo baada ya kutembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe
katika Maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
CHUO
Kikuu Mzumbe, kimewaalika wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na elimu ya
juu kujisajili chuoni hapo ili waweze kuja kuwa chachu ya kuendelea
kukuza uchumi wa kati.
Akizungumza
katika maonyeshao ya 15 ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja wa
Mnazi mmoja jinini Dar es salaam, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe,
Profesa Lugano Kusiluka amesema, kozi zote zinazotolewa na Chuo hicho ni
za muhimu sana hasa katika kukuza uchumi wa nchi.
"Unapozungumzia
nchi kuingia kwenye uchumi wa kati unakuwa unazungumzia utawala,
biashara sheria ujasiliamali na mengineyo ambayo yote tunayofundisha
hapa chuoni... hayo ni mahitaji ya zamani na ya sasa kwa sababu hakuna
mahali popote duniani unapoweza kuendesha uchumi bila ya kuwa na
wataalamu wa fedha na wanasheria, biashara na wajasiriamali.
Amesema
Chuo hicho cha Mzumbe kimebobea katika masuala ya utawala, biashara
uchumi, ujasiliamali, tehama nk. Na kwamba wahitimu wake wengi wamekuwa
wakifanya kazi katika sekta mbali mbali za umma na binafsi nchini.
Aidha,
Kasulika amewakaribisha watanzania wote vijana ambao wamemaliza shule
za Sekondari hivi karibuni, wenye cheti, kuomba kujiunga na Chuo hicho
kwani wamejitayarisha kwa ajili ya kuwapokea na kuwapa taaluma
itakayowezesha kujiendesha kimaisha.
Ameongeza
kuwa Chuo kimekuwa kikifanya maboresho katika matawi yake yote ambapo
katika Tawi la Mbeya kunajengwa bweni litakalokuwa na unauwezo wa
kuchukua wanafunzi 900.
"
Kwenye kampasi kuu maboresho yanaendelea ambapo sasa tunajenga bweni
linaloweza kuchukua wanafunzi elfu moja ambalo tunatarajia mwishoni mwa
mwaka huu litaanza kutumika kwani serikali iko katika hatua za mwisho
kukamilisha na poa Chuo kiko katika hatua ya ujenzi wa madarasa mapya
katika matawi yake yote yatakayoweza kuchukua wanafunzi wa ziada elfu
moja.
"Tunaboresha
sana miundombinu katika Chuo chetu ili kiendane na umaarufu wa jina la
Chuo hiki katika maeneo ambayo tunatoa huduma.
Amesema,
kuanzia mwaka huu Chuo hicho tawi lililopo Upanga ambalo kwa miaka
mingi walikuwa wakitoa shahada ya uzamili (masters) sasa wataanza kutoa
shahada ya kwanza.
Pia
amesema, Chuo kupitia tawi la Dar es Salaam, wanajenga madarasa mapya
eneo la Tegeta ma tunaomba wanafunzi kujitokeza kwa wingi na kujisajili
ili waweze kupata elimu ya juu iliyo bora.
No comments :
Post a Comment